Na.Mwandishi Wetu,Lindi.
Watumishi wa umma mkoani Lindi wametakiwa kufanya kazi kwa mujibu wa viapo vyao ili kuepuka mambo yanayosababisha kushusha imani ya wananchi kwa watumishi wa umma.
Wito huo umetolewa na katibu tawala wa mkoa wa Lindi, Abdallah Chikota alipokuwa anafungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa mkoa wa Lindi (sekretarieti ya mkoa) kilichofanyika leo katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi. Chikota alisema watumishi wa umma hawanabudi kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria za utumishi kwa na viapo wa vyao, kwani maadili kwa baadhi ya watumishi wa umma yameporomoka
Alisema ingawa wanatakiwa kuwa ni mfano wa kuigwa kwa uadilifu na uaminifu, lakini baadhi yao ni vigumu kuwatambua na kuwatofautisha na watu wasio watumishi, kutokana kukiuka maadili utu. Hivyo wamekuwa ni mfano mbaya kwa jamii inayowazunguka katika maeneo wanayofanyia kazi.
Alisema baadhi ya watumishi licha yakuwa sio waaminifu, lakini hata mavazi, matendo na kauli zao zinawaondolea uwezekano wa kutambuliwa ni watumishi wa umma mbele ya wananchi. Alisema watumishi wanatakiwa kuepuka matendo yote yanayokwenda kinyume na kanuni, taratibu, miongozo na sheria za utumishi wa umma na viapo vyao."ukifika kwenye ofisi zetu ni vurugu tupu,wenzetu nchi nyingine wanaonafahari kushindana kufanya kazi kwa faida ya nchi zao" lakini sisi utamkuta mtumishi anafika ofisini anaanza kuperuzi simu kwa ajili ya wasap,anatoka kwenye ofisi yake anakwenda kwenye ofisi ya mwenzake anapigakelele na vicheka kiasi cha kusikika kwenye ofisi nyingine,kufurahi unafarahi wewe wengine inawahusunini," alionya na kushangaa Chikota.
Katibu tawala huyo ,amewataka kuheshimu na kutoa ushirikiano kwa mamlaka nyingine ikiwamo Taasi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambayo ipo kisheria.Hata hivyo baadhi yao, hasa wasio waaminifu wanaichukia.
Alisema taasisi hiyo ipo kwa mujibu wa sheria,hivyo hawana budi kuipa ushirikiano kila inapohitajika kufanya hivyo kwani inatekeleza wajibu wake."kama hutaki wakufuate fuate uwe mwaminifu,badala ya kuwachukia na kuwaona ni maadui,"alisema.
Hata hivyo RAS huyo aliwataka maofisa wa TAKUKURU na askari wa jeshi la polisi waache tabia ya kuwatisha mashahidi wanapowahitaji kwenda kutoa ushahidi.Kwa madai kuwa baadhi yao wamekuwa wakiwaita mashahidi kwa vitisho na ukali kama watuhimiwa wa kosa husika wakati wanajua kwamba mashahidi hao ni muhimu kwao ilikushinda kesi dhidi ya washitakiwa. Mwanasheria wa TAKUKURU mkoa wa Lindi, Dismas Muganyizi aliwataka watumishi kutoa taarifa zinohusiana na vitendo vinavyofanywa na watumishi wenzao wanaofanya kazi kinyume cha taratibu na sheria ikiwamo rushwa. Huku akianisha makosa mbalimbali ambayo yapo kwenye sheria ya Kuzuia na kupambana na rushwa.