HII NDIO ADHABU ALIYOPEWA MCHEZAJI WA CHILE, BAADA YA KUMFANYIA UHUNI UWANJANI EDINSON CAVAN

Beki kutoka nchini Chile, Gonzalo Alejandro Jara Reyes amefungiwa michezo mitatu, baada ya kubainika alikua chanzo cha vurugu zilizojitokeza kati yake na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Edinson Cavanni wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali ya michuano ya ukanda wa Amerika ya kusini (Copa America).
Edinson Cavanni
Kamati ya maandalizi ya fainli za Copa America iliyo chini ya shirikisho la soka ukanda wa Amerika kusini CONMEBOL, ilikutana jana nchini Chile, na kubaini Jara alionyesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu dhidi ya mpinzani wake.

Kamati hiyo imeridhia kumfungia michezo mitatu beki huyo wa klabu ya Mainz 05 ya nchini Ujerumani, sambamba na kumtoza faini ya dola za kimarekani 7,500.

Kufuatia maamuzi hayo Jara, ataanza kutumikia adhabu yake kwa kukosa mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Peru ambao utachezwa alfajiri ya kesho, kisha mchezo wa fainali ama mshindi wa tatu.

Mchezo mwingine wa tatu utakaomuhusu Jara katika adhabu yake ni ule wa kusaka nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2018.

Kamati ya CONMEBOL, ilijiridhisha kufanyika kwa kitendo cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na Jara, kwa kuangalia picha za televisheni ambapo ilibainika beki huyo mwenye umri wa miaka 29 alimfanyia kitendo kiovu Edinson Cavani sehemu za makalio.

Baada ya kitendo hicho, Cavani ambaye anaitumikia klabu bingwa nchini Ufaransa PSG, alihamaki na kumsukuma kwa hasira Jara na ndipo muamuzi wa mchezo alipomuadhibu kwa kumuonyesha kadi nyekundu.
Chanzo::Timesfm
Previous Post Next Post