"TUTAHAKIKISHA NEC INAKUWA NA SAUTI KWA SERIKALI YAKE" ASEMA KINANA

Abdulrahman Kinana
Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameahidi kuwa watafanya mageuzi ambayo yanaifanya Halmashauri Kuu ya Chama (NEC) hicho kuwa na nguvu katika kuisimamia serikali yake.

Akihutubia jana mjini Mwanza, alisema hiyo ni kuongeza uwajibikaji wa viongozi na watumishi ndani ya Serikali ili vyeo walivyo navyo viwe vya utumishi na sio vya utukufu ili kuongeza ufanisi ndani ya Serikali.

Alisema watu wakishapata vyeo na madaraka wanajisahau na vyeo vinageuka vyao na si vya wananchi. Alisema umezuka ugonjwa wa ‘mheshimiwa’ kwa maana mtu akishapata cheo hata kama alikuwa kwenye jamii, anajiita mheshimiwa.
Previous Post Next Post