Abdulaziz Ahmeid Mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten Akifanya mahojiano na mwandishi wetu Nyumbani kwake.
Na AHMAD MMOW-LINDI
Hivi karibuni mwandishi wa habari
wa kituo cha televishen cha channel ten, Abdulaziz Ahmeid akiwa mjini Lindi Mbele
ya waandishi wa Habari wenzake wa vyombo mbalimbali vya habari alitangaza nia
ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi ili ateuliwe kugombea ubunge katika
jimbo la Lindi mjini, ambalo kwa sasa mbunge wake ni Salum Barwany wa CUF-Chama
Cha Wananchi.
Mtandao huu ulifanya mahojiano
na Abdulaziz, Mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa na mtendaji wa Chama Cha Mapinduzi
katika mikoa mbalimbali, Marehemu Ahmed Abdulaziz.
Yaliyojiri kwenye mahojiano hayo
yaliyofanywa na mwandishi wetu Ahmad Mmow, fuatilia na soma makala haya:-
Mwandishi: Abdulaziz Wasomaji
na mimi mwenyewe napenda kujua historia yako japo kwa ufupi.
Abdulaziz: Mimi ni kijana mwenye
haki ya kuitwa kijana, maana nina miaka 41 tu,nilizaliwa mwaka 1974, Nina Mke na
Watoto watatu.
Elimu yangu ni ya kidato cha nne
ambayo niliipata katika shule ya sekondari ya Mkonge iliyopo hapa Lindi Kuanzia
mwaka 1990 hadi 1993.
Elimu ya msingi nilisoma katika
shule tofauti Maana Marehemu baba Yangu alikuwa mtumishi wa Chama Cha
Mapinduzi, alikuwa mhasibu wa CCM mkoa. Kwa hiyo alipokuwa anahamishwa kutoka
kituo kimoja na kuhamia kituo kingine tulikuwa tunahama wote.
Mwandishi: kwahiyo elimu ya msingi
ulipata katika shule gani?
Abdulaziz: Kabla ya shule ya
msingi nilianza na elimu ya awali, chekechea katika shule ya Parish
inayomilikiwa na kanisa katoliki pale Mtwara.
Baba kwa muda huo alikuwa mhasibu
wa CCM mkoa wa Mtwara.
Ilikuwa 1979 hadi 1980. Nakumbuka
Mwaka 1981 nirudia tena kusoma elimu ya awali katika skuli ya Kidutani, Zanzibar
baada ya marehemu baba kuhamishiwa mkoa
wa mjini magharibi kama Mhasibu wa CCM Mkoa.
Mwaka 1982 nilianza darasa la
kwanza katika skuli ya Kisiwandui hukohuko Zanzibar(1981-1985).
Mwaka 1985 Kwa Mapenzi ya Mungu Baba
alifariki ghafla akiwa ofisini
Kwake, ofisi ya CCM Kisiwandui Baada ya kifo hicho Tulilazimika kurudi kijijini
kwetu Mchinga Wilaya na Mkoa wa Lindi
Hivyo Baada ya kifo cha Marehemu baba ambaye alizikwa katika kijiji
hicho, Mimi, dada yangu Salma Ambae nae alifariki 1995 pamoja ndugu yangu ALLY
Tulibaki kijijini.
Yaani Mwandishi Hapa nalazimika
sana kukishukuru sana Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu kwa kukodi Ndege Aina ya
Forker ya shirika la ATC kuleta maiti ya baba Kutoka Unguja hadi kiwanja cha
Ndege Cha Kikwetu na Ndege hiyo ililala kiwanjani hapo hadi siku ya Pili kuwasubiri
waombolezaji waliotoka Unguja kuja Kuzika ili kuwarudisha hakika ulikuwa
Mchango mkubwa kwa waliokuwa karibu na marehemu pamoja na waliokuwa wakifanya
nae kazi pamoja.
Pia Jitihada zilizofanywa na Bi
Fatma Mikidadi ambaye alikuwa ni mke wa baba yangu mkubwa Marehemu Basheikh
Mikidadi (MNEC) Kabla ya kifo chake 1984 Bi Fatma Mikidadi alifika kijijini akiwa
Mratibu wa elimu Lindi aliwasiliana na Marehemu Mama Yangu na akatuchukua mimi na dada yangu ili tukaendelee
na masomo katika shule ya msingi ya stadium iliyopo katika mji wa
Lindi.
Namshukuru sana alipotoa wazo la kurudia darasa toka la nne na kuanza
Darasa la Tatu Aug 1985 ambapo Nilisoma na kumaliza elimu ya msingi katika
shule hiyo mwaka 1989.
Mwandishi; Umetangaza nia ya kuomba
ridhaa ya chama chako ili uteuliwe kugombea ubunge. Lakini jimbo hili lina
mbunge, na kwa mujibu wa CCM muda wa wanachama wake kutangaza nia haujafika.
Je wewe umeamua kupuuza marufuku
hiyo ya CCM unayotaka kuomba ridhaa yake?
Abdulaaziz: Mwandishi hili ni
Jimbo huru Bwana:Nikweli CCM kimepiga marufuku kutangaza nia kabla ya muda
kufika, lakini siyo kwa majimbo yote.Bali kwa majimbo yale ambayo wabunge wake
wanapitia CCM tu Hivyo Jimbo la Lindi mbunge wake hatokani na CCM, ruksa
kutangaza Nia na kuanza Mambo ili mradi usivunje kanuni na kuchochea
Migawanyiko. Lakini wapo wanachama wametangaza nia ya kugombea urais wakati rais
aliye madarakani hajamaliza muda wake hii inatokana na Rais huyo kutogombea
Tena kipindi kijacho.
Kwa hiyo sijakiuka taratibu, kanuni
wala sheria za CCM.
Mwandishi: Nini kimekusukuma kugombea
ubunge, tena katika jimbo la Lindi mjini badala ya jimbo la Mchinga ambalo kwa
mujibu wa maelezo yako, ndiyo nyumbani kwenu?
Abdulaaziz: Kwanini nataka kugombea Lindi
mjini badala ya Mchinga Mwandishi Hapa Lindi mjini ni nyumbani pia,uliza wana
Lindi watathibitisha Na hata wazazi wangu Mchinga ni kwao ila makazi na maisha
yao ni Mjini Lindi labda Kuhusu kilichonisukuma kutaka kugombea ni Kuwepo kwa maendeleo
duni na hafifu ya jimbo la Lindi mjini.
Hayo ni matokeo ya Kukosa
Uwakilishi ikiwamo mbunge ambae Mwaka 2010 wananchi wakiwemo wana CCM Kujenga
Imani nae kwa kubadilika na kutoa ridhaa kwa CUF
Mimi niliomba ridhaa ya chama
changu kugombea, lakini kura hazikutosha kwenye kura za maoni. Hata hivyo kero
za wananchi hazijapata uvumbuzi hadi sasa.
‘Nilipotafakari nakujipima
nikagundua naweza kuzishugulikia changamoto na matatizo yaliyopo.
Mwandishi: Umesema jimbo la
Lindi linachangamoto nyingi, Unaweza kuzitaja japo kwa uchache?
Abdulaziz: Changamoto ni nyingi
ikiwamo kuporomoka kwa kiwango cha elimu katika jimbo la Lindi na mkoa mzima wa
Lindi kwa jumla.
Mkoa huu uliwahi kushika nafasi
ya kwanza kwa ufaulu wa watoto wa darasa la saba. Lakini tumeporomoka na kuwa
mkiani. Tatizo ni uongozi uliopo kutokuwa na mikakati sahihi ya kulipatia
ufumbuzi tatizo hili kwa kuanza kutafuta sababu.
Viongozi waliopo ikiwamo mbunge
hawaoneshi kusikitishwa wala kujali hali hii. Hivi jiulize kama wangekuwa
serious kulitafutia uvumbuzi isingewezekana baadhi ya shule za hapa Lindi mjini
hazina vyoo vya kutosha, hali inayosababisha waalimu na wanafunzi kushirikiana
choo hii imejionyesha katika shule ya sekondari ya Angaza....
Migogoro isiyokwisha na ya mara
kwa mara ndani ya baraza la madiwani la
halmashauri ya manispaa ya Lindi.
Badala yake mbunge ambaye ni sehemu
ya madiwani anakuwa nichanzo cha migogoro.
Mwandishi: Kama chama chako
kikikupa ridhaa na hatimae kuwa mbunge. Je utayawekea kipambele mambo gani?
Abdulaziz: Kimsingi jimbo la
Lindi linachangamoto nyingi, lakini mimi nitaanza kwanza kwa kusimamia nidhamu ya matumizi ya fedha
katika manispaa. pili kuunganisha makundi yanayo hasimiana na kusababisha migogoro
isiyo na tija kwa wananchi. Baada ya hapo nitaanza na miundo mbinu ya
barabara, maji, afya na elimu, jambo ambalo litakuwa miongoni mwa mambo ya awali
kuyashugulikia.
Kwani elimu ndiyo msingi wa
maisha. Kwajumla changamoto ni nyingi, lakini ili kufanikiwa kuzishugulikia ni
ushirikiano nitakaopewa na wana Lindi. Ukiwa kiongozi nilazima uwe kiongozi wa watu, ambao
nao wanajibu wakukupa ushirikiano.
Mwandishi: Ungozi mzuri unategemea uzoefu. Wewe
unazoefu wowote?
Abdulaziz: Kuwa mwandishi wa habari ni uzoefu pia kwani
ninachanganyika na makundi mbalimbali na watu wenye rika nyadhifa na kazi
mbalimbali nasijawahi kulalamikiwa katika utendaji na utekelezaji wa majukumu
yangu ya uandishi wa habari.
Pia nilipokuwa sekondari nilikuwa
katibu wa umoja wa vijana wa ccm tawi la sekondari ya Mkonge. Utaona kuwa
nimeanza kuwa kiongozi nikiwa umri mdogo. Kama hiyo haitoshi tangu nijiunge na
kuwa mwanachama wa klabu ya waandishi wa habari nimekuwa kiongozi nikianza na ukatibu
msaidizi mwaka 2008, wanachama walionesha imani na kunichagua kuwa mwenyekiti wao, kulikotokana na umahiri wangu hususani katika UMOJA kwa Vilabu vya waandishi wa habari nchini.
Mwandishi: Kwahiyo unawahaidi
nini wananchi wa jimbo la Lindi iwapo watakuchagua nakua mbunge wao?
Abdulaziz:Watarajie maendeleo ya
kasi yatakayotokama na rasilimali zilizopo Lindi na mji wa lindi unakua kwa
kasi na kuna kilasababu nyingi lakini kubwa zaidi raslimali ya gesi asili
iliyogunduliwa katika kanda hii. Gesi imepandisha thamani ya ardhi na maliasili
nyingine.
Kwahiyo kinachohitajika nikiongozi makini tu, lazima Lindi itasonga
mbele na kuondokana na udumavu uliopo sasa. Inasikitisha kuona raslimali
zilizopo zinazalisha migogoro badala ya maendeleo. Utakumbuka kuna mgogoro wa
ardhi umesumbua sana hapa Lindi. Hali hiyo imetokana na kukosekana uongozi
makini.
Mwandishi: Mara nyingi watu
wanapoomba uongozi wamekuwa natabia ya kuhaidi mambo mengi mazuri, lakini
wakichaguliwa wanageuka. Hilo lipoje kwako iwapo utachaguliwa?
Abdulaziz: Hilo lipo na bado ndilo
lililowafanya wana CCM na wananchi wa
Lindi, mwaka 2010 wamchague mgombea wa upinzani ambaye alihaidi mambo mengi
mazuri, wananchi wa Lindi walijazwa matumaini. Lakini baada ya kuchaguliwa amewageuka
anatenda kinyume na alivyokuwa amehaidi.
Kwangu haitakuwa hivyo, ndiyo sababu nimesema
mafanikio ya kiongozi yanatokana na ushirikiano uliopo na wananchi ikiwemo namna
yeye mwenyewe atakavyowashirikisha pamoja na kupokea ushauri.
‘Hayo yatafanyika ukiwa karibu na
wananchi naomba Wasiwe na shaka, mimi nitabaki kuwa mtu wa Lindi nanitaendelea
kuishi Lindi.
Mwandishi: Naamini wana CCM
wenzako na wananchi wa Lindi, wamekusikia. Nakutakia mafanikio katika harakati
zako za kutaka kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Lindi mjini.
Abdulaziz: Ahsante, nashukuru.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.