TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN) YATOA RAMBIRAMBI KWA MWANAHABARI WA FAMILIA YA WATU SITA WALIOFARIKI KWA AJALI YA MOTO

Tanzania Bloggers Network - TBNMwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network - TBN ), Joachim Mushi (kulia) akitoa pole na kisha kukabidhi ubani wa fedha shilingi laki tano (500,000/-) jana zilizotolewa kwa mwanahabari wa Kitulo FM ya Njombe Bw. Conrad Mpila kama pole toka TBN baada ya kupoteza ndugu watano wa familia moja katika ajali ya moto iliyotokea hivi karibuni na kuua watu sita eneo la Kipunguni jijini Dar es Salaam. Katikati ni mmoja wa wajumbe wa TBN, Dotto Mwaibale. TBN ilishiriki katika mazishi ya marehemu hao sita waliozikwa jana katika makaburi ya Airwing, Dar es Salaam.
Tanzania Bloggers Network - TBN"Tupo nawe katika wakati huu mgumu..." anasema Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network - TBN ) Bw. Joachim Mushi wakati anakabidhi ubani huo
Tanzania Bloggers Network - TBN"Pole sana Conrad", Bw Mushi anamfariji mfiwa. 
Picha na Francis Dande.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post