YOTE YALIYOSIKIKA KUHUSU HALI YA BOBBI KRISTINE, HII NI TAARIFA RASMI ILIYOTOLEWA NA FAMILIA YAKE

Bobbi Kristina
Bado kuna utata kuhusu kinaachoendelea juu ya afya ya Bobbi Kristina, mtoto wa pekee wa Marehemu Whitney Houston, mengi yanaendelea kuzungumzwa kuhusu hali yake huku wengine wakisema kuwa leo ni siku ambayo familia hiyo imeruhusu madaktari kumtoa mashine ya kupumulia ambayo aliwekewa toka siku ambayo alifikishwa hospitali baada ya kukutwa akiwa ameanguka ndani ya bafu, Georgia Marekani.

Baada ya yote kusikika familia ya Bobbi huyo imeamua kutumia kampuni ya wanasheria wao kutoa maelezo rasmi kuhusu kila ambacho kimesikika kuhusu hali ya mtoto huyo, taarifa hiyo imekanusha uvumi wote uliowahi kusikika ikiwemo ishu ya kumtoa mipira ya kupumulia siku ya leo ambapo ni siku ambayo mama yake alifariki.

Katika taarifa hiyo ya Wanasheria wa familia hiyo wamesema wanaangalia namna ya kuwachukulia hatua wote waliotoa taarifa za uongo ikiwemo waliosema walizungumza na wahusika wa familia hiyo kitu ambacho sio kweli.

Whitney Houston na Bobbi Kristine
Marehemu Whitney Houston akiwa na mtoto wake Bobbi Kristine wakati akiwa mdogo.

TMZ, The National Enquirer, The Atlanta Journal Constitution na the Daily Mail ni sehemu ya vyombo vya habari ambavyo vimelaumiwa kwa kuandika taarifa za uongo.

Bado hakuna taarifa rasmi ambayo familia hiyo imetoa kuhusu hali ya mtoto huyo, leo inatimia miaka miaka mitatu tangu afariki Whitney Houston ambaye alikutwa pia ameanguka bafuni.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post