Unknown Unknown Author
Title: FUATILIA TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA...!!!! SNEIJDER, GUNDOGAN NA RAPHAEL VARANE WANYEMELEWA NA MAN UNITED
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
DIRISHA LA UHAMISHO liko wazi tangu Januari 3 na litafungwa hapo Februari 2 na kama kawaida ya kipindi hiki zipo tetesi na uvumi mwingi. ...
DIRISHA LA UHAMISHO liko wazi tangu Januari 3 na litafungwa hapo Februari 2 na kama kawaida ya kipindi hiki zipo tetesi na uvumi mwingi.
Nigel De Jong, Ilkay Gundogan, Wesley Sneijder
Nigel De Jong                            Ilkay Gundogan                            Wesley Sneijder

FUATILIA:
Toka Germany, zipo habari kuwa Borussia Dortmund wako tayari kumuuza Ilkay Gundogan kwa Manchester United kwa sababu tu hawataki Mchezaji huyo aondoke mwishoni mwa Msimu bila wao kuambua Senti.

Mkataba wa Gundogan unakwisha Mwezi Julai na Dortmund hivi sasa wako taabani mkiani mwa Ligi ya Bundesliga na hili limefanya Mastaa wao wengi kufikiria kuhama ikiwa ni pamoja na Marco Reus.

Baada ya Wakala wa Mholanzi Wesley Sneijder kusema ile Dili ya Kiungo huyo kwenda Juventus kutuka Galatasaray imekufa sasa ipo minong’ono kuwa Mchezaji huyo ataenda Man United kwa Dau la Puni Milioni 8 ambazo ni mara mbili ya lile Juve walilotaka kulipa.

Sambamba na Sneijder, Mholanzi mwingine ambae anasemekana yupo njiani kwenda Old Trafford ni Nigel De Jong kwa sababu tu AC Milan wanataka kuijenga upya Timu yao.

Raphael Varane
Kutoka huko Spain, zipo taarifa kuwa Sentahafu wa Real Madrid, Mfaransa Raphael Varane anapiganiwa na Klabu za England, Chelsea na Man United, na Dau lake linakadiriwa kuwa Pauni Milioni 20.

Beki huyo mwenye Miaka 21 hana furaha kuichezea Real kwa vile hana namba ya kudumu kwani Kocha Carlo Ancelotti huwapa namba Pepe na Sergio Ramos na kumuacha yeye akicheza Mechi 5 tu za La Liga Msimu huu.

Nae Wilfried Bony, Staa kutoka Ivory Coast, amedaiwa kuishinikiza Klabu yake Swansea City imuuze huku Klabu kadhaa kubwa zikimuandama.

Radamel Falcao
Nae Staa wa Colombia, Radamel Falcao, amevumishwa kwenda Juventus ingawa Klabu yake ya sasa, Man United, ambako yuko kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu, imedokeza itaamua hatma yake Mwezi Aprili.

Mkopo wa Falcao kwa Man United una kipengele cha kumbakiza Old Trafford kwa kudumu.

Kiungo wa Southampton, Morgan Schneiderlin, amefuta matumaini ya Klabu kadhaa, zikiwemo Arsenal naTottenham, za kumnasa Mwezi huu Januari, baada ya kusema hahami hadi mwishoni mwa Msimu.

Virgil van Dijk
Nao Sunderland wanatayarisha Ofa ya Pauni Milioni 8 kumnunua Beki wa Celtic Virgil van Dijk ambae pia amedokezwa kuwaniwa na Louis van Gaal wa Man United.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top