Unknown Unknown Author
Title: YANGA YASHINDA MECHI ZOTE 3 KOMBE LA MAPINDUZI, BAADA YA USHINDI MWEMBAMBA DHIDI YA SHABA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Yanga imemaliza hatua ya makundi kwa kuwa na pointi 9 baada ya kupata ushindi wa tatu mfululizo. Yanga imeifunga Shaba bao 1- 0 katika me...
Andrey Coutinho
Yanga imemaliza hatua ya makundi kwa kuwa na pointi 9 baada ya kupata ushindi wa tatu mfululizo. Yanga imeifunga Shaba bao 1- 0 katika mechi ngumu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Pamoja na kushambulia sana na kukosa sana, Yanga walilazimika kusubiri hadi dakika ya 86 wakati Andrey Coutinho alipofunga bao kwa kichwa akiunganisha krosi ya Simon Msuva.

Yanga walipoteza nafasi zaidi ya tano za wazi za kufunga kupitia kwa Mrisho Ngassa, Simon Msuva na Amissi Tambwe.


Katika halli isiyo tegemewa Mashabiki wa timu hiyo walivamia kwenye lango la Shaba na kubeba glavu za akiba za kipa wa timu hiyo, Bakari Shaweji na kwenda kuzitupa nje ya Uwanja. huku imani ya kishirikina zikidaiwa dakika kumi baadaye Yanga ilipata bao dakika ya 86 kupitia kiungo wake Mbrazili Adrey Countinho


Hata hivyo, mashabiki wawili walikamatwa na Polisi na kupelekwa kituoni.

Kwa matokeo Hayo, Yanga SC itamenyana na JKU katika Robo Fainali keshokutwa usiku Uwanja wa Amaan, mchezo ambao utatanguliwa na mechi kati ya KCCA na Polisi Saa 9:00 Alasiri, Azam FC na Mtibwa Sugar Saa 11:00.


Robo Fainali ya kwanza itachezwa kesho Saa 2:15 Usiku Uwanja wa Amaan, kati ya SImba SC na Taifa ya Jang’ombe.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Edward Charles, Rajab Zahir, Kevin Yonean, Said Juma ‘Kizota’/Salum Telela dk59, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Hassan Dilunga dk81, Danny Mrwanda/Kpah Sherman dk59, Mrisho Ngassa/Amisi Tambwe dk59 na Andrey Coutinho.

Shaba FC; Bakari Shaweji, Robert Daniel, Juma Mwalimu, Bakari Kidarusi, Hassan Shaaban, Shekha Khamis, Kassim Kiondo, Suleiman Ally, Said Sinde, Mohammed Nyasa na Hamisi Ramadhani/Suma Ozil dk83.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top