MENINAH: NAOGOPA MAPENZI YATAVURUGA MUZIKI WANGU

Mwimbaji wa Bongo Flava aliyewahi kuwa mshiriki wa BSS, Meninah Ladivah akifanya mahojiano katika kipindi cha Hatua Tatu leo.
Meninah akiwa studio na mtangazaji anayeongoza kipindi cha Hatua Tatu, Times Fm, Maryam Kitosi.

Mwimbaji wa Bongo Flava aliyewahi kuwa mshiriki wa BSS, @MeninahLaDiva  amesema anaogopa kuwa katika uhusiano wa mapenzi kwa sasa anaamini mapenzi yatavuruga muziki wake.

Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm, @MeninahLaDiva ameeleza kuwa hivi sasa yuko single na hajawa na mpango wa kuingia katika uhusiano kutokana na sababu hizo.
“Kwa sasa niko Single naangalia kazi yangu kwanza... Nikiingia kwenye mahusiano kazi yangu itakuwa shaghala bagala.” Amesema Meninah.
Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa mwimbaji huyo ana ukaribu na @DiamondPlatnumz lakini alikanusha na kueleza kuwa hajawahi hata kuwa na ukaribu na mkali huyo.

Unaweza kuwa umeshasikia na unaamini @MeninahLaDiva  yuko kwenye uhusiano na….. Lakini msikilize pia yeye. 
“Unajua watu wanaamini ukiwa msichana mzuri basi ni lazima uwe katika uhusiano!”
Meninah ameachia wimbo mpya unaoitwa ‘Pipi ya Kijiti’.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post