BREAKING NEWS:: WATU ZAIDI YA WANNE WAHOFIIWA KUFA KATIKA AJALI YA GARI ENEO LA MTAMA LINDI

lindiyetu news
Ajali Imetokea jioni hii eneo la Kijiji cha Mtama Lindi Vijijini katika Pacha ya kuelekea Newala ikilihusisha gari aina ya TDI (DEFENDER) ilikuwa inatokea katika maonyesho ya Nane nane yaliyofikia kilele leo jioni katika viwanja vya Ngongo Mjini Lindi.
Ajali hiyo inasemekana imesababishwa na Mbuzi alie kuwa anakatiza barabara na Dereva alivyojaribu ku mkwepa tu akayumba na kuwagonga wafanyabiashara waliokuwa pembezoni mwa Barabara hiyo na kuishia kutumbikia mtaroni.
Hadi sasa Taarifa iliyo rasmi watu wanne wamefariki dunia kutokana na ajali hiyo.
Endeleo kuwa nasi kwa Habari Zaidi na Picha zaidi.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post