Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanafunzi hao pamoja na wazazi wao, walisema kuwa waliamua kufika ofisi za Mkuu wa Mkoa ili kujua hatima yake, baada ya kuona hawapewi majibu ya kuridhisha kutoka kwa viongozi wa chini yake.
Walisema tangu wizara itangaze majina kwa ajili ya kujiunga kidato cha tano wiki mbili zilizopita, wameshangazwa kuona wanafunzi kutoka shule hiyo hawajapangiwa kwa ajili ya kuendelea na masomo katika ngazi hiyo, licha ya kuwa na ufaulu mzuri.
Wanafunzi hao ambao wamepata alama za daraja la kwanza hadi tatu, hawajui hatima yao kutokana na wizara husika kushindwa kuwapangia shule kwa ajili ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano.
Nao wazazi ambao waliambatana na watoto wao hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (CHADEMA) kwa nia ya kutafuta suluhu ya suala hilo, walisema kuwa tangu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutangaza majina ya wanafunzi waliofaulu kwa ajili ya kidato cha tano na shule walizopangiwa, hakuna majina ya watoto wao.
Mmoja wa wazazi hao, Lawrance Shimo, alisema baada ya kufuatilia kwa kina ikiwemo kuuliza uongozi wa shule, walibaini kuwa katika shule hiyo hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyepangiwa shule kwa ajili ya kuendelea na kidato cha tano, licha ya kuwa na ufaulu wa alama mzuri.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.