Unknown Unknown Author
Title: WACHEZAJI WA TIMU YA DAR YOUNG AFRICA KUNUFAIKA NA MRADI WA NYUMBA ZA BEI NAFUU ZA NSSF KIGAMBONI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Yanga ...
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Yanga wakati wa mkutano wao wa kuzungumzia umuhimu kwa wachezaji hao kumiliki nyumba zao,uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akifafanua jambo mbele ya wachezaji wa timu ya Yanga na viongozi wa timu hiyo (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Timu ya Yanga,Beno Njovu akieleza nia ya Timu yake ya kutaka kuwawezesha wachezaji wao waweze kuwa na Nyumba zao wenyewe.
Watendaji wakuu wa NSSF
Sehemu ya Uongozi wa Timu ya Yanga chini ya Kocha Mkuu,Marcio Maximo.
Wachezaji wa Yanga wakipitia vipeperushi walivyopewa juu mradi wa nyumba za bei nafuu za NSSF.
Baadhi ya Wachezaji wa Yanga wakifatilia kwa makini maelezo waliyokuwa wakipewa.

NA.MWANDISHI WETUKLABU ya yanga imeingia makubaliano ya kununua nyumba kwa ajili ya wachezaji wake na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) .

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika mkutano maalum na wachezaji hao Mkurugenzi wa uendeshaji NSSF, Crescentius Magori amewaambia wachezaji hao kuwa "kijana mjanja mjini ni yule ambaye ana miliki nyumba ama ardhi kuliko magari" huku akiwahamasisha wachezaji wa Yanga kuchangamkia ununuzi wa nyumba hizo ambazo ziko katika mradi wa makao mapya katika kijiji cha Dege Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Sisi tuko tayari kuwapa fomu na kwenda kuwaonyesha nyumba hizo ambazo zimejengwa kisasa zaidi hivyo ningependa kuwashauri pindi mnapopata fedha zenu za mikataba mkitoa kiasi ili kuweza kuwa kati ya wamiliki wa nyumba hizo” alisema Magori.
“Endapo utaweza kumudu na kutoa kiasi cha sh. mil.8 taslimu na kulipa kwa miezi mitatu mfululizo unapewa NSSF wanamupa funguo na kuendelea kulipa kila mwisho wa mwezi hadi kwa miaka 15 unakuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo”alisema Magori.
Aidha aliongeza kwa kuwaambia wachezaji hao kwamba endapo utakufa ndugu anaweza kurithi nyumba hiyo. Huku akiwasisitiza wachezaji ambao bado hawajajiunga na NSSF kufanya hivyo mara moja ili waweze kujivunia matunda ya uchezaji wa mpira hapo baadaye.

Wakati huohuo Katibu wa Yanga Beno Njovu aliwaambia waandishi wa habari kwamba hayo ni mawazo ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji ambaye alizungumza na Mkurugenzi wa NSSF Ramadhan Dau ambapo wote kwa pamoja wameamua kuwawezesha wachezaji wa timu hiyo ili waweze kuwa na mali zao za kudumu hadi uzeeni.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top