Gari ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji likiwa eneo la Mwanyamala mapema leo mchana,ambapo moto mkubwa umezuka na kuteketeza nyumba nzima na mali zilizokuwemo,ambazo thamani yake haikujulikana mapema,tukio hilo limetokea maeneo ya Mwananyamala jirani na hospitali ya Mwananyamala.
Baadhi ya watu wakishuhudia tukio la Moto lililotokea mapema leo mchana,ambapo moto huo umeteketeza nyumba nzima na mali zilizokuwemo,ambazo thamani yake mpaka Globu ya jamii inaondoka eneo la tukio haikufahamika.
Baadhi ya Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea kuzima moto kwenye moja ya chumba cha nyumba hiyo,Mashuhuda waliokuweo kwenye tukio hilo wanaeleza kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyokuwa imetokea kwenye moja ya chumba ndani ya nyumba hiyo.
Majirani walijitokeza kuzima moto kwa kutumia ndoo kama uonavyo pichani
Mabati yaliyobahatika kutetekea kwa moto yakitolewa nje.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea kuzima moto.
Baadhi ya raia wema pia walijitokeza kusaidia kuuzima moto huo.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.