Unknown Unknown Author
Title: VAN GAAL MAN UNITED AMPA ROBIN VAN PERSIE WIKI TATU ZA MAPUMZIKO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mimi na likizo tu! Robin van Persie amepewa wiki tatu za mapumziko baada ya kumalizika kwa kombe la dunia. ROBIN van Persie amepewa l...

robin van persie
Mimi na likizo tu! Robin van Persie amepewa wiki tatu za mapumziko baada ya kumalizika kwa kombe la dunia.
ROBIN van Persie amepewa likizo ya wiki tatu na kocha wa Manchester United, Louis van Gaal na hataungana na kikosi cha klabu hiyo kwa safari ya America.
Mshambuliaji huyo wa Uholanzi aliweka wazi kuwa anahitaji likizo baada ya Wadachi kumaliza katika nafasi ya tatu ya kombe la dunia nchini Brazil.
Hii ni tofauti kwa Wayne Rooney, kwani yeye amelazimika kukatisha likizo na kuungana na timu katika maandalizi ya kabla ya msimu.
Van Persie alikosa mechi 8 mwishoni mwa msimu uliopita na alikuwa anakaribia kumaliza bila kufunga katika mechi ya jumamosi usiku dhidi ya wenyeji Brazil.
van gaal with Rvp
Kocha mpya wa Manchester United, Louis van Gaal ameamua kumpa likizo nyota wake.
Mshambuliaji huyo alicheza dakika 548 katika mashindano yote na Van Gaal ameona anahitaji kupumzika ili kurudi na nguvu mpya kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England.
"Nahitaji likizo," alisema Van Persie. "Yalikuwa mashindano magumu. Kila mechi nilicheza kadiri niwezavyo. Ndivyo ilivyokuwa, haikuwa rahisi".
rvp wife
Mke wa Robin Van Persie akiwa katika visiwa vya Bardos sambamba na Mumewe RVP 
Wakati huo huo imekuwa tofauti kwa Rooney, mchezaji mwenzake na Van Persie .
Maamuzi hayo ya kwanza kwa Van Gaal akianza kazi Man United, yanakuwa na utata ingawa yanaonekana kuwa sahihi.
Van Persie alikosa mechi 27 za Man United msimu uliopita, na hivyo ikipewa likizo anaweza kupata muda mzuri wa kukusanya nguvu.
Alionesha kiwango kizuri katika fainali za kombe la dunia. Nyota huyo mwenye miaka 30 alifunga mabao manne likiwemo la kichwa maridadi dhidi ya Hispania katika mchezo wa ufunguzi na alikuwa mshambuliaji chaguo la kwanza la Van Gaal.

Pia Van Gaal amekuwa na uhusiano mzuri na Van Persie na anatarajia kumpa majukumu ya unahodha wa United badala ya Wayne Rooney.
Mwishoni mwa wiki, Van Gaal alimsifu sana nyota wake.
"Kama unajua alitoka wapi na amefanya nini, unachoweza kufanya ni kumpongeza tu," alisema kocha huyu mwenye miaka 62.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top