Unknown Unknown Author
Title: REAL YAENDA USA NA KIKOSI DHAIFU!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
LEO hii Real Madrid wameruka kwenda Marekani kushiriki International Champions Cup wakiwa na Kikosi dhaifu ambacho kina Wachezaji 9 toka Ti...
LEO hii Real Madrid wameruka kwenda Marekani kushiriki International Champions Cup wakiwa na Kikosi dhaifu ambacho kina Wachezaji 9 toka Timu yao B, Castilla.
real madrid players
Mbali ya kuwakosa Álvaro Morata na Casemiro ambao Juzi tu wamehama, Real haina hata Mchezaji wao mmoja aliecheza Kombe la Dunia huko Brazil.

Wachezaji wa kwanza wa Real waliokuwa Brazil ambao watajumuika Kikosini Jumatano huko Los Angeles ni Wachezaji wa Spain, Xabi Alonso, Iker Casillas na Sergio Ramos, pamoja na Luka Modric wa Croatia.

Kisha, Siku mbili baadae, watafuatia Wachezaji wa Portugal, Fábio Coentrão, Cristiano Ronaldo na Pepe, lakini Ronaldo atakuwa kwenye Mazoezi maalum binafsi akiendelea kupona Goti lake.

Kundi jingine la Wachezaji wa Kombe la Dunia wa Real ni lile la Wachezaji wao kutoka France, Raphaël Varane na Karim Benzema, na hawa wamepangiwa kurudi Likizo Agosti 1.

Wachezaji waliosalia ni wale Timu zao zilikutana kwenye Fainali ya Kombe la Dunia huko Brazil, Angel Di Maria aliekuwa na Argentina na Toni Kroos na Sami Khedira waliokuwa na Germany, na hawa watajiunga na Real hapo Agosti 5 toka kwenye Likizo zao.

International Champions Cup

MAKUNDI  KUNDI A:

-Manchester United
-AS Roma
-Real Madrid
-Inter Milan

KUNDI B
-AC Milan
-Olympiacos
-Manchester City
-Liverpool

RATIBA**Saa zikitajwa ni za Bongo
Ijumaa Julai 25

03:00 Olympiacos CFP v AC Milan

Jumamosi Julai 26
23:10 Manchester United v AS Roma

Jumapili Julai 27
1:00 Real Madrid CF v Inter Milan
23:00 AC Milan v Manchester City

Jumatatu Julai 28
02:00 Liverpool - England v Olympiacos CFP

Jumatano Julai 30
02:00 Manchester United v Inter Milan
05:15 Real Madrid CF v AS Roma

Alhamisi Julai 31
02:00 Manchester City v Liverpool

Jumamosi Agosti 2
20:00 Inter Milan v AS Roma
22:00 Olympiacos CFP v Manchester City
23:06 Manchester United v Real Madrid CF

Jumapili Agosti 3
01:30 Liverpool v AC Milan

FAINALI
Jumatatu Agosti 4

Mshindi Kundi A v Mshindi Kundi B
>>SOKA IN BONGO

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top