Unknown Unknown Author
Title: TANGAZO LA KUJIUNGA NA JKT KWA WALIMU NA WAHITIMU KIDATO CHA SITA 2014
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TANGAZO MUHIMU KWA WALIMU NA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014 KUHUSU KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWEZI ...
mwenge
TANGAZO MUHIMU KWA WALIMU NA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014 KUHUSU KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWEZI SEPTEMBA 2014

1. Awamu ya pili kwa vijana watakaojiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mujibu wa Sheria itaanza rasmi tarehe 11 septemba, 2014 na itahusisha makundi yafuatayo:-

Walimu wote ngazi ya cheti (GATCE) 2014 ( Waliomaliza mwaka 2014).
Walimu elfu tatu (3,000) ngazi ya Diploma (DSEE) (Waliomaliza mwaka 2014).
Vijana waliomaliza kidato cha sita mwaka 2014 waliopangwa awamu ya pili ambao hawana sifa za kujiunga na vyuo vya elimu ya juu (Vyuo Vikuu).

2 . Vijana waliomaliza kidato cha sita mwaka 2014 ambao walipangwa kujiunga na JKT awamu ya pili na wana sifa za kujiunga na elimu ya vyuo vya juu (Vyuo Vikuu) wanatakiwa kuandika barua ya
kuahirisha kuhudhuria mafunzo ya JKT mpaka hapo watakapomaliza masomo yao. Barua hizo ziwe zimefika Makao Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa kabla ya tarehe 15 Agosti, 2014. Barua zinaweza kutumwa kwa:-

Anwani
Mkuu wa JKT
Makao Makuu ya JKT
P.o.Box 1694, Dar es Salaam

E-mail: info@jkt.go.tz (barua iwe na sahihi ya mhusika na ifanyiwe “scanning”).
Barua iletwe na mhusika Makao Makuu ya JKT.

3. Awamu ya tatu ambayo itahusisha walimu wa Diploma (DSEE) itaanza mwezi Januari 2015.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA
-------
WALIMU-CHETI KWENDA VIKOSI MBALIMBALI
BUROMBOLA - KIGOMA
RWAMKOMA - MUSOMA
MSANGE - TABORA
KANEMBWA - KIGOMA
RUVU - PWANI
OLIJORO - ARUSHA
MGAMBO - TANGA
MARAMBA - TANGA
MAFINGA - IRINGA
MLALE - SONGEA
MTABILA - KIGOMA
MAKUTOPORA - DODOMA

WALIMU-DIPLOMA KWENDA VIKOSI MBALIMBALI
BUROMBOLA - KIGOMA
MSANGE - TABORA
KANEMBWA - KIGOMA
RUVU - PWANI
OLIJORO - ARUSHA
MGAMBO - TANGA
MARAMBA - TANGA
MAFINGA - IRINGA
MTABILA - KIGOMA
MAKUTOPORA - DODOMA

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top