Unknown Unknown Author
Title: NI RASMI JUVE YAMSAINI EVRA!, STEVEN GERRARD ASTAAFU ENGLAND!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
PATRICE EVRA anaondoka Manchester United na kuhamia Juventus baada ya kudumu Miaka 8 na Nusu Old Trafford kwa mujibu wa habari zilizothibit...
PATRICE EVRA anaondoka Manchester United na kuhamia Juventus baada ya kudumu Miaka 8 na Nusu Old Trafford kwa mujibu wa habari zilizothibitishwa na Klabu zote mbili.
Evra
Evra anaondoka Man United mara tu baada ya Meneja mpya Louis van Gaal kumsaini Kijana wa Miaka 19 Luke Shaw kutoka Southampton kuziba pengo lake.

Juventus imempa Evra Mkataba hadi 2016 na watailipa Man United Euro Milioni 1.2 kwa mikupuo miwili na Euro Laki 3 zaidi ikiwa Msimu ujao watafuzu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Evra alitoa ujumbe kwa Mashabiki wa Man United na kuwaambia: 
“Baada ya kufikiri sana nimeamua sasa ni muda muafaka kuondoka Manchester United. Ni uamuzi mkubwa mno katika maisha yangu ya Soka kwa sababu Klabu hii, na Siku zote itabaki hivyo, ipo moyoni mwangu!”
Akiwa na Man United, Evra alicheza Mechi 379 na kufunga Bao 10 katika Misimu 9.

Evra, anaetoka France, alijiunga na Man United Januari 2006 kutoka Monaco ambako, akiwa na Miaka 24 tu, alikuwa Nahodha wao na kucheza Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2004.

Mwanzoni Evra alikuwa na wakati mgumu akiichezea Man United na katika Mechi yake ya kwanza kabisa dhidi ya Man City waliyofungwa 3-1, alitolewa wakati wa Haftaimu.

Lakini baada ya Miezi 6 tu alimpora namba Gabriel Heinze na kuisaidia Man United kutwaa Ubingwa Msimu wa 2006/07.
Evra
Akiwa na Man United, Evra alitwaa Ubingwa wa England mara 5, Ligi Cup 3, UEFA CHAMPIONZ LIGI na Klabu Bingwa ya Dunia.

Pia amewahi kuteuliwa kwenye Timu ya Mwaka ya PFA [Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa] mara 3, kwenye Misimu ya 2006/07, 2008/09, 2009/10, na Mwaka 2009 alikuwemo kwenye Kikosi cha Mwaka cha UEFA na kile Kikosi cha Dunia cha FIFA FIFPro.

Wakati Nemanja Vidic alipokuwa majeruhi, Evra ndie alikuwa akikaimu Nafasi ya Nahodha wa Mnchester United.

STEVEN GERRARD ARASMI ATANGAZA KUSTAAFU KUSHEZEA TIMU YA TAIFA

NAHODHA wa England Steven Gerrard amestaafu kucheza Mechi za Kimataifa baada ya kuichezea England mara 114.
Steven Gerrard
Gerrard, mwenye Miaka 34 na ambae alianza kuichezea England Mwaka 2000 kwenye Mechi waliyoifunga Ukraine 2-0, aliichezea England kwa mara ya mwisho huko Brazil Mwezi uliopita walipotoka Sare 0-0 na Costa Rica kwenye Mechi ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia.

Akitangaza habari hizi, Gerrard alisema:
“Nilisikia raha muda wote niliochezea Nchi yangu. Hii ni Siku ya huzuni kwangu.”
Kwenye Mechi hizo 114 alizocheza alifunga Bao 21 na kushiriki Mashindano makubwa 6.

Gerrard ataendelea kuichezea Klabu yake Liverpool ambayo alicheza nao Mechi yake ya kwanza kabisa Mwaka 1998 dhidi ya Blackburn Rovers.

Gerrard, ambae amekuwa Nahodha wa England mara 38, ndie Mchezaji wa 3 kwa kuichezea England mara nyingi akiwa nyuma ya Kipa Peter Shilton, Mechi 125, na David Beckham, Mechi 115.

Gerrard ametoa shukrani zake kwa wote aliokuwa nao wakati aliichezea England.

Nae Mwenyekiti wa FA, Chama cha Soka England, Greg Dyke, amemsifia Gerrard na kumwita ni Nguli wa kweli wa England.
>> SOKA IN BONGO

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top