NEWS:: NDEGE NYINGINE YAPOTEA, "AIR ALGERIE"

LOGO
Maafisa wa masuala ya anga nchini Algeria wanasema wamepoteza mawasiliano na ndege ya shirika la ndege la Air Algerie, iliyokuwa katika anga ya Sahara. Shirika la habari za Algeria limesema ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kwenda Algiers na kupotea kwenye rada takriban dakika 40 baada ya kupaa kutoka jijini Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso. Air Algerie imesema imeanza shughuli za dharura kuitafuta. Inadhaniwa kuwa na abiria 110 na wafanyakazi sita. Njia ya ndege hiyo ni kupitia nchini Mali ambapo kuna mzozo unaendelea upande wa kaskazini.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post