Unknown Unknown Author
Title: MANCHESTER UNITED IMEIBAMIZA LA GALAXY GOLI 7 - 0. CHELSEA WATOA DROO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kuna kitu nakiona kinakuja pale Old Trafford ujio huu wa Van Gaal ni tofauti kabisa na anguko lile la David Moyes. Kipindi kama hik...
Kuna kitu nakiona kinakuja pale Old Trafford ujio huu wa Van Gaal ni tofauti kabisa na anguko lile la David Moyes.
MAN UNITED
Kipindi kama hiki Moyes alianza kibarua kwa kichapo cha bao 1-0 toka kwa kombaini ya Hongkong, muda mfupi uliopita Van Gaal kashusha kichapo cha paka mwizi kwa Galaxy katika dimba la Rose Bowl.

Amewatumia Jones, Smalling na Evans kama walinzi huku Shaw na Valencia wakicheza kama wing-backs kikosi kimeonekana kubalance vizuri mno huku Ander Herrera akianza kuthibitisha thamani yake nadhani mpira umetabasamu mara nyingi zaidi ulipofika miguuni kwake.

Waswahili wanasema siku nzuri huonekana asubuhi, naiona Manchester haswa tena ya kiajax na kibayern siyo ile ya kieverton.

Bao za Manester United zilifungwa na Danny Welbeck, Dakika ya 13, Rooney (Penati) 41’, na jingine 45’, Reece James, 62’ & 84’ na Ashley Young, 88’ & 90’.

Mechi inayofuata kwa Manchester United ni hapo Jumamosi Julai 26 dhidi ya AS Roma Sports Authority Field, Denver ikiwa ni Mechi ya Kundi A kugombea International Champions Cup.

RZ PELLETS WAC 1-1 CHELSEA
Wakati Chelsea inatoka Sare 1-1 kwenye Mechi ya Kirafiki na RZ Pellets huko Austria hapo Jana, Meneja wao José Mourinho amesema yupo tayari kumhuzunisha mmoja wa Makipa wao.
CHELSEA

Petr Cech Jana alicheza baada ya kuwa nje kwa muda mrefu alipoumia Msimu uliopita
lakini Chelsea wanakaribia kumkaribisha Kipa Thibaut Courtois aliekuwa huko Atletico Madrid kwa Mkopo kwa Misimu Mitatu.

Cech aliumia Mwezi Aprili kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top