KUAHIRISHA SAFARI YA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA KUANZIA LEO JUMANNE JUNI 10, 2014

TRL
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na kutetereka kwa daraja la reli kati ya stesheni ya Ruvu na mchepuko wa reli ya Ruvu kwenda Mruazi usiku wa kuamkia leo, umeamua kusitisha kwa muda huduma ya usafiri wa abiria hadi ukarabati wa daraja utakapokamilika.

Tokea asubuhi ya leo Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu na Wahandisi waandamizi na Mafundi ujenzi walifika katika daraja hilo lililopo km 82/5 na kulifanyia tathmini kuwa linahitaji kuimarishwa ili lirejee katika kiwango cha usalama kuruhusu treni za abiria kupita.

Kwa taarifa hii wananchi na wateja wa TRL na wananchi kwa jumla ambao walikuwa wasafiri kwenda bara kwa treni ya leo Juni 10, 2014 wanatakiwa kufika katika stesheni zilizokaribu nao ili warejeshewe nauli zao ili watafute usafiri mbadala. Aidha Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Aman KisamfuDar es SalaamJuni 10, 2014

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post