![Ajali yatokea rondo Ajali yatokea rondo](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhGtR_scLK3d7JshIoAFbHih5wh9rbrFkretQWeSe8wAF6tDPw1_w58BbMBwxxCNIfUjCQobsjbe69yPAyVOKxXgrg0dIJm87xWiAwcaKQLtkQm03SgRN2lLKwcu3h1gOlKGbAHfLJJtjo/s1600/AJALI+RONDO+5.jpg)
Watu 3 wamefariki Dunia baada ya Magari mawili yenye tela kila moja kuacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya watu hao na kujeruhi wengine wawili katika ajali iliyotokea Jana Huko Tarafa ya Rondo wilaya ya Lindi Mkoani Lindi.
![Ajali yatokea rondo Ajali yatokea rondo](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjSPBRxBc-rytE0-a2B8wBZQM0KuPyBs0TjZWyzlBtcM1hfEzjAKjwMsq0qkyLa0YsWz5jAZkDJyU6yx7TUkQV2JhlvkbX87UQa7Nub6oTl5FvSW_dgLQH6A1KPfDmS3LuXeCjzZlrQyxE/s1600/AJALI+RONDO+3.jpg)
Ajali hiyo Iliyohusisha gari aina ya HOWO lenye Usajili T270BZU na Tela na T260AZU pamoja na Lori aina HOWO T871 BTH Tela T 626 BTT yote yaliacha njia.
![Ajali yatokea rondo Ajali yatokea rondo](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYCtoltNp51Tt5f8gu9-xcGCuqTTnGlJdpyvZ8zW50UKM4xnxU9J9wHArkPciSEymGAs3eRMTiB845gWhE5E4_DOUox78R3FTm0D90mODdLqOMFblgWnzbI9aIiLGJsAPGrWhnx990AkA/s1600/AJALI+RONDO+4.jpg)
![Kamanda Mzinga Kamanda Mzinga](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNDOUw2RLgDvQI09Q1B6RYhapLbgJfBttFyymc4zOOs00MowbHhZEQ6dwLYwNa6gEJGmpBTf9-OIC3CF5Alcst_g97y2nq1jA290Mest2TP3NbsbxEaeDeoc4U_osKwj5AZPx-PPrJzY4/s1600/AJALI+RONDO+1.jpg)
![Ajali yatokea rondo Ajali yatokea rondo](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh4wESwXllRaorn7NjF9qeFtFJYeHFP2VoW_rFFonshEediH9DXagOHAlcg1uG6bi_lr_yaRMIM_1pIN2IIfVi_pRFaJeCgrlyaG4jaiEMwgvYLEjfNBJH6sxAoOU3HOn_ZXaA9uHk9DGU/s1600/AJALI+RONDO+7.png)
MATUKIO YA MWISHO WA WIKI MKOANI LINDI
Wakazi wanne wa wilaya za Nachingwea, Ruangwa na Manispaa ya Lindi, wamefariki dunia katika matukio tafauti, likiwemo mtu anayesadikiwa kuwa na matatizo ya akili kuwapiga vikongwe wawili mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani hapa.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani hapa, Regina Mzinga, vifo hivyo vimetokea mei 27 na 31 mwaka huu, katika wilaya tatu kati ya tano zilizopo mkoani hapa.
Amewataja marehemu hao kuwa ni, Mwanahawa Said (65) na Bakari Maurusi
(70) wakazi wa kijiji cha Mpiruka, wilaya ya Nachingwea, Mahamudu Issa
wa kijiji cha Mbagala, wilaya ya Ruangwa na Hadija Seifu (10) mkazi wa
mtaa wa kariakoo Manispaa ya Lindi.
Mzinga amefafanua kwa kueleza kwamba,Mwanahawa na Maurusi wamepoteza
maisha yao mei 27 mwaka huu,mchana baada ya kupigwa kwa rungu kichwani
na mtu aitwae Agnes Mathayo,anayedaiwa kuwa na matatizo ya
akili,wakati ndugu zao wakiwa mashambani.
"Hawa vikongwe wawili na huyu muuwaji Agnes walibaki nyumbani,wakati
jamaa zao wengine walikwenda kushughulikia mazao mashambani mwao" Alisema Mzinga.
Kamanda huyo wa Polisi mkoani Lindi, amesema tayari mtuhumiwa Agnes Mathayo ameshakamatwa na kushikiliwa kituo cha wilaya kilichopo mjini Nachingwea, akisubiri kufanyika kwa utaratibu wa kumpeleka Hospitali ya kupima akili kabla ya kumfikisha Mahakamani.
Akasema Mahamudu Issa, ambaye alikuwa ni mwalimu mstaafu amefariki mei 27/2014, saa 1:30 baada ya kuamua kujinyonga kwa kujitundika juu ya mti aina ya mkorosho uliokuwepo karibu na nyumba yake kwa madai ya ugumu wa maisha, kutokana na kuishiwa fedha za malipo ya kustaafu.
Katika tukio la tatu, kamanda Mzinga akasema mtoto Hadija Seifu amepoteza uhai wake mei 31 mwaka huu, saa 3:05 asubuhi,baada ya kugongwa na gari ndogo aina ya Hiace katika barabara kuu itokayo mjini Lindi kwenda mikoa ya Mtwara na Ruvuma.
Ameeleza kuwa Hiace hiyo yenye namba za usajili T. 354 CRM ilikuwa ikiendeshwa na Abdull Mohamedi (32) mkazi wa mtaa wa kariakoo Manispaa ya Lindi, na kwamba dereva huyo atafikishwa Mahakamani muda wowote baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.