Katika kuelekea msimu mpya wa ununuzi wa korosho mwaka 2025/2026, Chama cha Ushirika cha RUNALI kimetangaza rasmi ratiba ya minada ya zao hilo, ambapo jumla ya minada 11 imepangwa kufanyika kupitia AMCOS mbalimbali katika wilaya za Ruangwa, Liwale na Nachingwea.
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, mnada wa kwanza utaanza rasmi tarehe 2 Novemba 2025, katika ofisi kuu za RUNALI zilizopo Wilayani Nachingwea, na utakuwa ndio mwanzo wa msimu wa mauzo ya korosho kwa mwaka huu.
RUNALI imesisitiza kuwa maandalizi yote muhimu yamekamilika, huku wakulima wakihimizwa kufuata utaratibu uliowekwa ili kuhakikisha minada inafanyika kwa uwazi, haki na tija kwa wote.
Tags
Lindi
