Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva, ametangaza
mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika
katika sekta ya elimu ndani ya halmashauri za Manispaa ya Lindi na Mtama, mkoa
wa Lindi. Amebainisha kuwa uwekezaji huo umekuwa na mchango mkubwa katika
kuboresha ufaulu wa wanafunzi.
Akizungumza ofisini kwake, Mwanziva alisema kuwa juhudi mbalimbali zinafanywa ili kuhakikisha watoto wa kike wanapewa kinga dhidi ya ukatili wa kijinsia, ili waweze kufikia malengo yao na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Tags
Lindi