Unknown Unknown Author
Title: "VIKAO VYA CHAI MARUFUKU" MWIGULU NCHEMBA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Katika kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima, Mwigulu alisema fedha zitapelekwa kwenye mambo muhimu. Kama hali ngumu na wananchi wanalazimik...
Katika kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima, Mwigulu alisema fedha zitapelekwa kwenye mambo muhimu.Kama hali ngumu na wananchi wanalazimika kula mlo mmoja kwa siku, walioko ofisini pia wanaweza kukosa chai ili kuwezesha mambo mengine muhimu yafanyike kwa wakati.
mwigulu nchemba
"Tunachotaka wizara zibane matumizi tubaki na yale yenye umuhimu. Tunaomba wenzetu kwenye wizara watuunge mkono ili kuhakikisha bajeti hii inakwenda na wakati kwa maana ya mgawo wa fedha badala ya kuchelewa kama ilivyo sasa" alisema Migulu.

Mwigulu alisema jambo lingine la nne litakalozingatiwa ni usimamizi wa fedha zinazopatikana kwani pamoja na makusanyo kidogo, lakini pia kuna uvujaji."Tunataka fedha inayopatikana na kupangiwa kazi fulani itumike kwa shughuli iliyokusudiwa kama tutahakikisha tunasimamia na kudhibiti matumizi yake" alisema.

Alisema lengo ni kuhakikisha matumizi yaendane na thamani kwa uhalisia wa jamboNaibu Waziri huyo wa fedha alisema eneo la tano ambalo litaangaliwa ni eneo la fedha ambazo hazitokani na kodi bali zinachangwa na wananchi na wadau wengine katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.Alisema eneo hilo ni muhimu mbalo serikali inaona kuna haja ya kulisimamia vizuri ili kuhakikisha fedha za wananchi zinatumika vizuri.

"Kuna wakati wananchi wanachanga fedha kwa ajili ya ujenzi wa zahanati au jengo la ofisi. Wakati mwingine fedha zao zinakuwa nyingi kuliko zinazotolewa na serikali.Unakuta wananchi wamejenga jengo baadae anakuja mhandisi anasema ujenzi wake haukufata vigezo hivyo livunjwe. Hili litaangaliwa haiwezekani fedha za wananchi zikapotea bure ndio maana tumeweka kipaumbele katika eneo hili," alisema.

Alisema upotevu wa fedha ni upotevu, hivyo serikali itakuwa makini katika fedha za umma zinazochangwa na wananchi katika miradi ya maendeleo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top