Unknown Unknown Author
Title: TANESCO HII NI AKILI AU MATOPE, KUFUNGA NYAYA JUU YA MTI BAADA YA NGUZO KUVUNJIKA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Njia Mbadala Baada ya Nguzo kuvunjika Nguzo iliyovunjika Kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni jijini Dar es salaam ambapo mvu...
Njia Mbadala Baada ya Nguzo kuvunjika
Nguzo iliyovunjika

Kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni jijini Dar es salaam ambapo mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na miundo mbinu mbalimbali .

Uharibifu mkubwa nawa hatari ni katika nguzo za umeme zilizo vunjika na baadhi ya nyaya zinazo pitisha umeme kushuka chini ambazo ni hatari kwa wananchi.

Katika eneo la Mlalakuwa mbele kidogo baada ya kulivuka daraja ukiwa unaelekea kawe pana nguzo tatu ambapo nguzo moja imevunjika kabisa na nyingine mbili zimelegea katika nguzo iliyovunjika ni mali ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) liliweza kufika katika eneo hilo wakachukua hatua ya kufungua nyaya za ile nguzo iliyo katika na kuzifunga juu ya mti ulio pandwa pembeni mti huo si mkavu ni mbichi.

Je shirika la umeme la Tanzania madhara ya umeme wananchi watayafahamu vipi wakati ninyi wenyewe wataalamu wa kazi hiyo mnatupotosha, pili sehemu mulipo fungia na nyaya zilipo legea ni sehemu watu wanapo ishi, hivi huku nikuwajali wateja wenu?

Tunaomba muchukue hatua haraka iwezekanavyo ili kuepusha madhara yanayo weza kujitokeza hapo baadae kwani ni hatari sana.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top