Super Eagles wamepangwa kundi A pamoja na Afrika ya Kusini, Sudan na timu nyingine ambayo itafahamika baada ya kuwa imefuzu kupata nafasi iliyobaki katika kundi.
Kanu ambaye hakuwahi kutwaa taji la AFCON akiwa kama mchezaji amesema "Hakuna timu katika kundi hilo iliyo na ubavu wa kuizuia Nigeria isifuzu, Super Eagles itamaliza ikiwa ya kwanza katika kundi".
Nyakati za kupoteza zimefikia mwisho tunakwenda kuongoza kundi na kuelekea Morocco kutetea ubingwa wetu. Tutakirudia kile ambacho tulikifanya Afrika ya Kusini mwaka 2013.
Tumerudi katika zama zetu za ubingwa na tutaendelea kuwa mabingwa katika michuano ijayo ya AFCON.
Kuelekea michuano ijayo ya kombe la dunia Kanu anasema "Michuano hiyo siku zote huwa ni migumu ndiyo maana huitwa kombe la dunia. Huu ni wakati wa kocha kuwajua vizuri wachezaji wake pamoja na mbinu atakazozitumia. Kitakachoibeba Nigeria ni maandalizi bora na umakini katika kila mchezo".
Wakati huo huo Kanu amemtaka kocha wake wa zamani Arsene Wenger kubadilika na kuendana na wakati ili kurejesha mataji klabuni hapo.
Anasema "Arsenal lazima waingie sokoni kununua wachezaji,lazima wawekeze. Ni muhimu kununua wachezaji sahihi katika wakati sahihi. Najua Wenger hataki kununua lakini ni vyema akafanya hivyo. Timu inahitaji wachezaji nyota hasa baada ya timu kuteteleka katika mechi kubwa za ndani na nje".
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.