Unknown Unknown Author
Title: SSRA YAKAMILISHA MAFUNZO MKOANI LINDI, WAANZA KUTOA ELIMU MKOA WA MTWARA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Mkoa wa Lindi.,Ludovick Mwananzila akipokelewa na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano SSRA,Bi Sarah Kibonde Msika alipowasil...

DSC_0004Mkuu wa Mkoa wa Lindi.,Ludovick Mwananzila akipokelewa na
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano SSRA,Bi Sarah Kibonde Msika alipowasili katika Ukumbi wa MM hotel kwa ajili ya Ufunguzi wa mafunzo kwa wajasiliamali Kupitia SIDO Lindi

DSC_0056Picha ya Pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa na baadhi ya washiriki
wa Mafunzo kwa wajasiliamali wa mjini Lindi walipokuwa wanajengewa Uwezo wa kujiunga na SSRA

DSC_0033Mkuu wa Mkoa wa Lindi akisoma hotuba ya ufunguzi wa semina
kwa wajasilamali wa Lindi ambapo aliwaasa kujiwekea akiba na kukopa kupita mifuko ya Hifadhi

DSC_0052Baadhi ya wajasiliamali waliohudhuria mafunzo hayo

Na Abdulaziz Video.Lindi
SERIKALI imeishauri mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa elimu kwa
wananchama ambao ni watumishi wa umma mkoani Lindi ili waondokane na dhana ya kustaafu utumishi wa umma kuwa ni mwisho wa maisha yao.

Mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akifunguwa semina ya siku moja ya wajasiliamali wa manispaa ya Lindi iliyoendeshwa na mamlaka ya usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA)kwa kushirikiana na Sido Mkoa wa Lindi .

Akifungua semina hiyo,Mwananzila Alisema kuwa watumishi hujiunga
kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila kupata elimu ya kutosha kiasi
inachangia mstaafu kuona mwingine anapata mamilioni ya fedha huku
mwingine akipata Kiasi kidogo kutokana na kuwepo katika mifuko tofauti hali inayomsababishia kutoweza kumudu maisha na hatimaye kupoteza uhai wake.

“hali inakuwa mbaya kwa mtumishi anapofikia anastaafu utumishi wa umma kutokana na mafao yake anayolipwa kutokana na kutojua awali na kushindwa kujiandaa mapema akiwa ktk utumishi wa Umma hivyo Mimi naona itolewe elimu kwanza kwa wanachama wa mifuko hiyo ngazi za wilaya, kata na vijiji na wanapostaafu wanakuwa wameshajuwa kiwango watakachokipata kuliko hali ilivyo mtumishi anaogopa kustaafu kwa kujiona amefika mwisho wa Maisha yake bila kufanya kazi”Alimalizia Mwananzila

Nae Bi Sarah Msika ,Mkuu wa kitengo cha Uhusiano SSRA aliwataka
wajasiliamali kujiunga na Mifuko ya Hifadhi kwa kuwa mifuko hiyo sasandio mkombozi kwa kunufaika na uwekaji wa akiba pamoja upatikanaji wa Mikopo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top