Unknown Unknown Author
Title: MAJANGA FC YAICHAPA LINDI SPORTS CLUB 2–1 NA KUFANIKIWA KUSONGA MBELE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Benchi la ufundi la timu ya Lindi Sports Club ambayo leo hii imepata matokeo mabaya ya kufungwa goli 2 – 1 katika uwanja wa Ilulu mjini Lind...

DSC06987Benchi la ufundi la timu ya Lindi Sports Club ambayo leo hii imepata matokeo mabaya ya kufungwa goli 2 – 1 katika uwanja wa Ilulu mjini Lindi na Majanga FC

DSC06992Bechi la Ufundi la Majanga Fc likionekana kuwa dhaifu kipindi mpira unaanza kwa kukosa wachezaji wa akiba, lakini waliweza kushinda mechi hiyo kwa Magoli 2 – 1 Dhidi ya Lindi Sports

Ligi Daraja la Tatu Ngazi ya Mkoa Imeendelea Leo hii katika Uwanja wa Ilulu Mjini Lindi Kwa Kuzikutanisha Timu za Lindi Sports Club yenye makao Makuu yake mjini Lindi na Majanga FC Yenye makao yake nje kidogo ya Mji katika sehemu moja iitwayo Nyangao.

Timu hizo Zilishuka Dimbani kuwania nafasi ya Tatu ya Kufuzu, huku nafasi ya Kwanza katika Ligi hiyo Ikiongozwa na Timu ya Kariakoo Fc ikifuatiwa na Timu ya Kusini Soccer.

Mpira ulikuwa wa ushindani mkubwa kwani wote wakihitaji point tatu muhimu lakini iliwachukua dakika 3 tu Timu ya Majanga Fc kuandika Bao la Kwanza kupitia kwa Mchezaji wao Machachari Maulidi Manyanya.

Hata hivyo Goli hilo La Majanga halikuwakatisha Tamaa Timu ya Lindi Sports kwani waliweza kusawazisha goli hilo Baada ya Beki wa Majanga kumuacha peki yake mshambuliaji Silaji Chamack huku akizani kaotea na bila ajizi aliuweka Mpira wavuni Na kubadilisha Ubao wa matangazo kwa kusomwa 1 – 1 hadi kipindi cha Mapumziko.

DSC06993Kocha wa Majanga Akiongea na Wachezaji wake kipindi cha Mapumziko huku matokeo yakiwa 1 – 1.

DSC06996Kocha wa Lindi Sports Club akitoa maelekezo kwa Vijana wake iliwaweze kupigana na kuibuka washindi katika mechi hiyo.

Kipindi cha Pili kilianza huku Mashabiki wakiishangilia kwa nguvu timu ya Majanga Fc kwani ikisemekana kuwa Timu ya Lindi Sports ilikuwa imepangwa ishinde mchezo huo ili iweze kufunzu lakini hali ilikuwa tofauti pale Mchezaji Tasilo Moses alipoiandikia Bao la Pili na Lakuongoza kupitia mpira wa Adhabu alioupiga kiufundi kuelekea katika kona post na kumshinda Mlinda mlango wa Lindi Spost na kutinga wavuni.

Mchezo ulikuwa na Tension kubwa Hasa kwa Lindi sports kwa kipindi hicho cha pili kwani walikuwa wamesha poteana kwa kuruhusu Mashambulizi ya hapa na pale na kufanya kucheza Rafu nyingi lakini Refa alionesha dhahiri kuwa beba, Lakini mbebeo huo ulifika kikomo Pale Mchezaji Laus Kazumari alipozawadiwa kadi Nyekundu kwa kosa la Kumpiga Ngumi Maiko Mlaponi Baada ya kumchezea rafu, Lakini Tukio la kushangaza Refa aliamua kuwatoa nje wote wawili kwa kadi nyekundu.

DSC06998Kamisaa akilindwa na Askari kwani tayari inasemekana mdaulikuwa umekwisha na bado refa alikuwa hataki kumaliza mpira, Pembeni ni kiongozi wa Timu ya Majanga Fc akilalamika.

DSC07002Hatimae Refa alimaliza mpira huo na kufanya matokeo kubaki Goli 2 kwa Majanga Fc na 1 Kwa Lindi sports Club na kuzima ndoto za timu ya Lindi Sports Kuendelea na Michuano hiyo

Hadi filimbi ya Mwisho wa mchezo baada ya refa kuchelewa kumaliza mchezo akitegea labda Lindi sports wataweza kurejesha bao hilo kwani Droo ilikuwa inawapa nafasi ya kufuzu lakini waapi hawakuweza kurejesha Goli hilo na Matokeo kubaki Lindi Sports 1 – 2 Majanga Fc

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top