LIGI KUU ENGLAND inaingia Kipindi kigumu cha Mechi mfululizo kwa Timu zote kucheza Mechi 3 dani ya Siku 5 kuanzia Desemba 26.
Boksing Dei, hadi Januari Mosi huku Vinara wa Ligi, Liverpool, wakianza kuivaa Man City Desemba 26 huko Etihad na kufuatia safari ya Stamford Bridge kucheza na Chelsea Desemba 29.
Liverpool wapo kileleni, wakiwa na Pointi 36 sawa na Arsenal, ila wao wako juu kwa ubora wa Magoli, lakini kuanzia wao hadi Nafasi ya 5 zinatenganishwa na Pointi 2 tu.
Mabingwa Watetezi, Man United, wao wako Nafasi ya 8 wakiwa Pointi 8 nyuma ya Liverpool.
JE WAJUA?
-Liverpool wameshindwa kuwa Bingwa katika mara zote tatu za mwisho walizoongoza Ligi wakati wa Krismasi.
-Mara hizo 3 ni 1990-91 walipomaliza Nafasi ya 2, Mwaka 1996-97 walipomaliza Nafasi ya 4 na 2008/09 walipomaliza Nafasi ya 2 nyuma ya Man United.
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, ambae Jumatatu Usiku Timu yake ilitoka 0-0 na Arsenal huko Emirates, ameeleza mbio za Ubingwa za safari hii ni kuwa haziaminiki.
Amesema: “Ni hali ya ajabu, ni Ubingwa ambao kila Mtu ana nafasi!”
Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema: “Ni hali ya mvuto. Timu ambayo itakuwa na mtiririko mzuri wa matokeo mazuri itakuwa juu!”
KIPINDI KIGUMU LIGI KUU ENGLAND:
ARSENAL | MAN UNITED | CHELSEA | |||
26 Des | W Ham v Arsenal | 26 Des | Hull v Man Utd | 26 Des | Chelsea v Swansea |
29 Des | Newcastle v Arsenal | 28 Des | Norwich v Man Utd | 29 Des | Chelsea v Liverpool |
1 Jan | Arsenal v Cardiff | 1 JAN | Man Utd v Tottenham | 1 Jan | S’pton v Chelsea |
SOUTHAMPTON | TOTTENHAM | LIVERPOOL | |||
26 Des | Cardiff v S’mpton | 26 Des | Tottenham v WBA | 26 Des | Man City v Liverpool |
29 Des | Everton v S’mpton | 29 Des | Tottenham v Stoke | 29 Des | Chelsea v Liverpool |
1 Jan | S’mpton v Chelsea | 1 Jan | Man Utd v Tottenham | 1 Jan | Liverpool v Hull |
MAN CITY | EVERTON | SWANSEA | |||
26 Des | Man City v Liverpool | 26Des | Everton v Sunderland | 26 Des | Chelsea v Swansea |
28 Des | Man City v Palace | 29 Des | Everton v S’mpton | 28 Des | Villa v Swansea |
1 Jan | Swansea v City | 1 Jan | Stoke v Everton | 1 Jan | Swansea v Man City |
Ligi itaendelea tena Desemba 26 wakati Timu zote 20 zitakaposhuka dimbani na kasha kucheza Mechi nyingine Desemba 28 na 29 na pia kutinga tena hapo Januari Mosi kwa Timu zote 20 kucheza.
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Liverpool | 17 | 11 | 3 | 3 | 42 | 19 | 23 | 36 |
2 | Arsenal FC | 17 | 11 | 3 | 3 | 33 | 17 | 16 | 36 |
3 | Man City | 17 | 11 | 2 | 4 | 51 | 20 | 31 | 35 |
4 | Chelsea FC | 17 | 10 | 4 | 3 | 32 | 18 | 14 | 34 |
5 | Everton FC | 17 | 9 | 7 | 1 | 29 | 16 | 13 | 34 |
6 | Newcastle | 17 | 9 | 3 | 5 | 24 | 22 | 2 | 30 |
7 | Tottenham | 17 | 9 | 3 | 5 | 18 | 23 | -5 | 30 |
8 | Man United | 17 | 8 | 4 | 5 | 28 | 20 | 8 | 28 |
9 | Southampton | 17 | 6 | 6 | 5 | 22 | 18 | 4 | 24 |
10 | Stoke City | 17 | 5 | 6 | 6 | 17 | 21 | -4 | 21 |
CREDIT TO SOKA IN BONGO
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.