WAFANYABIASHARA WAENDELEA KUGOMEA MASHINE ZA TRA, SASA NI MKOANI MOROGORO

clip_image002[15]Wafanya biashara wa Mkoa wa Morogoro wakiwa wamekusanyika wakijadili jambo.

Wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro wamegoma kufungua maduka leo wakitaka kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa Lengo la kushinikiza kukataa mashine za kieletroniki za mamlaka ya mapato tanzania.

Wafanya biashara hao wamegoma kufungua maduka tangu asubuhi wakishinikiza kuonana na mkuu wa mkoa jambo ambalo Mkuu wa mkoa amekubali na kuwaomba wateuliwe wawakilishi 8 kwa ajili ya kwenda kuonana naoa.

Baada ya wawakilishi kuteuliwa bado wafanyabiashara hao walishinikiza kuandamana mpaka nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa ndipo Jeshi la Polisi walipoingila kati .

clip_image002Jeshi la Polisi wakiwa barabara inayoelekea Kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Kulinda Amani na kuzuia maandamano yaliofanywa na wafanyabiashara hao muda huu.

clip_image002[5]Maduka yakiwa yamefungwa katikati ya Mji wa Morogoro 

clip_image002[7]Wafanyabishara hao wakiandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kushinikiza kuondolewa kwa mashine za Kieletroniki kwa madai kwamba ni kikwazo kikubwa katika biashara zao za kila siku

clip_image002[9]

clip_image002[11]

clip_image002[13]Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post