CHALENJI CUP 2013: DROO YAFANYIKA, KILI STARS WAKO NA ZAMBIA!

clip_image003CECAFA leo Mjini Nairobi imefanya Droo ya Mashindano ya Nchi za Afrika Mashariki na Kati,CHALENJI CUP, na kuipanga Kilimanjaro Stars, Timu ya Tanzania Bara, Kundi B pamoja na Waalikwa Zambia, Burundi na Somalia.

Nchi 11 Wanachama wa CECAFA, Shirikisho la Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati, zitashiriki pamoja na Wageni Waalikwa Zambia.

Zanzibar imepangwa Kundi A pamoja na Wenyeji Kenya, Ethiopia na South Sudan.

Mabingwa Watetezi Uganda wako Kundi C pamoja na Rwanda, Sudan na Eritrea.

Mashindano haya yatachezwa Nchini Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desema 12.

Mechi za Chalenji Cup Mwaka huu zitarushwa moja kwa moja na Vituo vya TV vya SuperSport, TV ya Taifa ya Uganda na TBC.

SOURCE: SOKA IN BONGO

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post