DOGO JANJA ATEMWA MTANASHATI ENTERTAINMENT

clip_image002Msanii mdogo aliyewahi kutamba katika tasnia ya muziki wa bongo fleva Dogo Janja amefukuzwa rasmi Mtanashati Entertainment,
Taarifa zilizofikia dawati letu la habari zinasema Dogo Janja amefukuzwa na Ostazi Juma Na Musoma baada ya kushindwana kitabia,
Hapo awali Dogo Janja aliwahi kuwa mwanakundi la Tip Top Connection lililo chini ya uongozi wa Madee hata hivyo alifukuzwa na kurudi kwao Arusha ambapo Ustazi Juma Na Musoma alimfuata na kumuweka kundini huku akimuhudumia katika kila jambo ambalo alitakiwa kupata kama mtoto na mwanamuziki pia.
Lakini Leo imefika tamati ya Ostazi Juma na kuamua kumuacha Dogo Janja aende zake.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post