DIVA AFUNGUKA KUHUSU NDOA NA PREZOO, HIKI NDO ALICHOKISEMA…

clip_image002Loveness Malinzi ‘Diva’ katika pozi na staa wa muziki wa Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’.

MTANGAZAJI wa Kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Redio,  Loveness Malinzi ‘Diva’ ameifungukia ndoa yake na staa wa muziki wa Kenya, Jackson  Makini ‘Prezzo’ kuwa haiko mbali kwani hatua waliyofikia ni nzuri.

Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni Diva alisema uhusiano wake na jamaa huyo hakuna wa kuutibua na anamshangaa msichana anayejitambulisha kwa jina la Boss lady anayedai ameingiliwa.
“Mimi namshangaa huyu dada anayeniandama kwenye mtandao toka aliposikia nipo na Prezzo, kwa kifupi kwa Prezzo nimefika na ndoa muda si mrefu utapita ili tuweze kuishi kama mke na mume” alisema Diva.
Diva alisema kuonyesha kuwa anakubalika hata kwenye familia ya Prezzo, aliongea na dada wa msanii huyo ambaye alimtuliza kwa kumwambia kuwa asisikilize maneno ya watu kwani yeye ndiye wifi yake wa ukweli.

CRDT: GPL

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post