Abdulaziz video,Ruangwa
MKUU wa wilaya Ruangwa mkoani Lindi Agnes Hokororo amemtaka mganga mkuu wa wilaya hiyo kuzitumia fedha za mfuko wa afya ya jamii kununulia dawa na vifaa tiba ili kuondoa upungufu wa madawa unazozikabili zahanati na vituo vya afya mara kwa mara katika wilaya hiyo.
Wito huo ameutoa wakati alipokuwa anafungua mafunzo ya elimu ya kata kwa kata kwa wadau na wanachama wa mfumo wa taifa bima ya afya na jamii uliofanyika wilaya ruangwa jana.
Hokororo alisema kuwa kero nyingi zinatolewa na jamii kuhusiana na huduma za mbovu zinazotolewa kwenye baadhi ya vituo vya afya, zahanati, inasababishwa na watendaji wasio waadilifu katika sekta ya afya kwa ukosefu wa dawa wilayani humo. alisema wapo watumishi wachache wenye malengo ya kuvipaka matope vituo vya kutolea huduma kwa sababu zao binafsi na imani potofu kuwa wanachama wa mfuko wa bima ya afya ni wagonjwa wanaopata huduma bure.
Alisema ni wajibu wa watoa huduma wa sekta ya afya kuwa wabunifu na kuzingatia wajibu wao, maadili na kufuata masharti yaliyowekwa na serikali ili waendelee kujijengea heshima na kulinda heshima za sekta ya afya.
Mkuu huyo wa wilaya pia alitoa wito kwa mfuko wa bima ya afya mkoani humo kushirikiana na halmashauri za wilaya kutoa elimu kwa wadau katika ngazi za vijijiji ili kutoa fursa kwa wadau walio vijiji kutoa kero zao kuhusiana ubora wa huduma za mfuk .
Sambamba na hilo aliwataka kuhakikisha kuendeleza ukaguzi wa vituo vya huduma ili uweze kuangalia hali na mfuko wa afya huduma, mazingira, ya vituo na idadi ya wafanyakazi katika vituo na hali ya vifaa tiba na vitendea kazi pamoja kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamiii.
Tags
HABARI ZA KITAIFA