Wafanyakazi wa hospitali ya Sokoine waliofanikisha uzimaji wa moto uliotokea
Na Abdulaziz,LindiHospital ya mkoa wa Lindi(Sokoine hospital) Imenusurika kuungua jana Usiku kutokana na Hitilafu ya Umeme Muuguzi wa Zamu, Bi Rehema mbinga alieleza kuwa Moto huo ulioanzia katika swichi ya Umeme uliweza kudhibitiwa Vema kufuatia huduma ya haraka ya kuzima moto iliyokuwepo hospital hapo.
Hata hivyo alieleza masikitiko yake kufuatia simu walizopiga katika
kikosi cha kuzima moto cha Manispaa ya lindi na mpokeaji kujibu majibu rahisi ya Acheni kutania nyie na kukata simu kila ikipigwa. Mwandishi tunashukuru kwa msaada wa wauguzi wenzangu tumefanikiwa kuzima moto huo ulioanzia katika dirisha la kutolea dawa ila fikisha ujumbe Kikosi cha zimamoto waache dharau na majibu rahisi wanapopigiwa simu vinginevyo watasababisha maafa leo sijui ingekuwaje na wagonjwa bila kuwahi kuzima moto..Alimalizia Bi Rehema
Tags
HABARI ZA KITAIFA