WATAKIWA KUCHAMKIA KUJIUNGA NA NHIF ,CHF

nhif 3
Abdulaziz video,Ruangwa
WANANACHI wa wilaya Ruangwa mkoani Lindi wameshauriwa kuchamkia fursa za huduma ya mfuko wa bima ya afya na afya ya jamii kwa kujiunga ili kupata huduma kwa lengo la kupunguza usumbufu wa kulipia mara kwa mara huduma hiyo.
Ushauri huo umetolewa mwenyekiti wa mafunzo Chande Razele wakati alipokuwa anafunga mafunzo ya elimu ya kata kwa kata kwa wadau na wanachama wa mfumo wa taifa bima ya afya na jamii uliofanyika wilaya ruangwa jana.
Chande alisema utaratibu unaofanywa na bima ya afya ya kukutana na
wanachama katika maeneo yao ya kazi ni utaratibu unaoonyesha nia
njema ,ushirikishaji na uwajibikaji katika sekta ya afya kwa lengo la
kuwakomboa wananchi hasa walio vijijini.
Chande alisema ni kieleleze tosha cha kutoa nafsi kwa wanachama wa
bima ya afya ya kukutana na kujadili maendeleo ya mfumo na suala zima la upatikanaji na utoaji wa huduma za matibabu kwa jamii.

Alisema hakuna budi wananchi kutumia frusa za mfuko wa bima ya afya katika kujipatia huduma za afya katika familia badala ya kuendeleza mfumo wa zamani wa kukata cheti dirishani.
“Tuache mambo ya kizamani ya kupata matibu kwa kutumia cheti ,
tubadilike sasa tutumie mpango wa bima ya afya na afya ya jamiii”
alisema chande.
Kwa upande wa msimamizi wa mfuko wa bima ya afya mkoani Lindi
Fortunata Kulaya mfuko kwa sasa una lengo la kuwasaidia wananchi
ambao hawako katika ajira rasmi ya serikali ili wapate huduma za
matibabu zilizo bora katika kaya kwa kipindi cha mwaka mzima baada ya kuchagia kiasi kidogo cha shs elfu kumi.
“Dhamira ya mfuko ni kupandua mtandao wa kuwa hudumia wananchi na ndiyo maana tunaonyesha jitihada za kufanya vikao na kukutana na wadau mbalimbali wa mijini na vijiji” alisema Kulaya.
Previous Post Next Post