Habari za Uhamisho wa John Rooney, Miaka 21, ambae ni Ndugu wa Straika wa Manchester United Wayne Rooney, zimethibitishwa na Bosi wa Barnsley Keith Hill.
Klabu ya mwisho kwa John Rooney kuichezea ilikuwa ni Klabu ya Marekani Orlando City ambayo ilikuwa ikicheza Ligi ya MLS.
Kabla ya kuichezea Orlando City, John Rooney alizichezea Klabu za Macclesfield Town ya England na New York Red Bulls ya huko Marekani.
Akiongelea Uhamisho huu wa John Rooney, Keith Hill alisema wamekuwa na Mchezaji huyo kwenye majaribio kwa Mwzi mmoja na wameridhika na kiwango chake.
Hata hivyo, Hill amesema hawategemei kukamilisha Uhamisho kabla ya Jumamosi ili kumruhusu kucheza Mechi yake ya kwanza ya Ligi na Klabu yake mpya Barnsley ugenini na Charlton.
Akifafanua, Hill alitamka: “John Rooney atasaini na sisi hadi mwishoni mwa Msimu. Ni Mchezaji mzuri na tunaweza kumuendeleza. Kwa sasa hatujui taratibu za Uhamisho wake zitachukua muda gani.”
Tags
Usajili Barani Ulaya