Picha na Habari na Abdulaziz Video,Ruangwa
Hayo yalielezwa na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa,Bi Agness Hokororo(Mb)alipokuwa akikabidhi trekta 4 aina ya Farmtrac (70E 60 HP 2WD)zilizonunuliwa Kupitia Mpango wa Maendeleo na Uendelezaji Kilimo wilayani(DADPS)Yenye thamani ya Tshs 160 Milioni ikiwa ni gharama ya Ununuzi na Usafirishaji hadi kufika wilayani humo. Akiongea na Wakulima hao baada ya Taarifa fupi ya makabidhiano iliyosomwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw Reubern Mfune,Mkuu wa wilaya aliwataka wakulima hao kuanzisha akaunti maalum ya kuyatunza matrekta hayo na mapato yote kuwekwa katika akaunti hizo ili kusaidia kumudu kujiendesha ikiwa pamoja na kuchangia asilimia 20 kwa ajili ya marejesho ya ununuzi wa trekta hizo ili kijiji kiweze kumilikishwa
Aidha Bi Hokororo aliitaka halmashauri hiyo kupitia maafisa Ugani kuhakikisha wanasaidia uendeshaji wa miradi hiyo huku wakiamasisha Jamii kuandaa mashamba yao ili yasiwe na Visiki ikiwa pamoja na kuhakikisha trekta hizo zinabeba mzigo uliolingana na uwezo uliopangwa kubebwa na trekta hizo ‘’Nataka muhakikishe kuwa trekta hizo ninazowakabidhi leo zinatumika kwa misingi ya kilimo na ziendeshwe na dereva mwenye leseni na aliepatiwa Mafunzo na si Vinginevyo’’’Alimalizia Hokororo.
Wakiongea na Mtandao huu baada ya kukabidhiwa Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Litama Kata ya Chinongwe Bw Rashid Mussa Nanjota pamoja na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nachinyimba kata ya Mandarawe wilayani humo waliishukuru Halmashauri hiyo kwa kusaidia jamii kupitia mpango huo wa kuendeleza kilimo baada ya wao kuibua mradi huo na
kukabidhiwa trekta hizo ambapo zitasaidia kuongeza kilimo kufuatia wilaya hiyo awali kuwa na trekta Moja ambalo lilikuwa alikidhi na kulazimika kukodi toka wilaya ya Nachingwea ambalo lilikuwa na Urasimu katika kupatika na kuwafanya kulima kwa gharama kubwa iliyofikia tshs Elfu 50 Mpaka 70 kwa eka Vijiji vilivyonufaika na Mpango huo ni Litama,Nachinyimba,Chilangalile na Michenga ambazo ziliwezeshwa kuibua miradi ya Kilimo na kupatiwa Mafunzo.
Tags
Lindi