Unknown Unknown Author
Title: HALMASHAURI ZA MKOA WA LINDI ZAAGIZWA KUTENGA MAENEO YA VIWANJA VYA MICHEZO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzira akikabidhi kikombe cha IMRAN Kwa Nahodha wa Timu ya Lunduno Fc baada ya kuibugiza  Timu ya Nachi...
image Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzira akikabidhi kikombe cha IMRAN Kwa Nahodha wa Timu ya Lunduno Fc baada ya kuibugiza  Timu ya Nachingwea kwa mikwaju ya penalti na kupata jumla ya mabao 6 kwa 5image Mratibu wa Mashindano ya IMRAN CUP ,,Abdulaziz Ahmeid akitoa taarifa fupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuhusiana na mashindano hayo yaliyoanza mwaka huu na kushindaniwa kila mwaka katika Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan
image Mdhamini wa Mashindano hayo Imran Traders,Mahamood Dhalla akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila na mratibu wa Mashindano hayo, Abdulaziz Ahmeid muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi katika uwanja wa Iluluimage
Halmashauri za Wilaya Na Manispaa katika Mkoa wa Lindi  zimetakiwa kutenga bajeti ya kutosha ya kuhudumia michezo hasa ujenzi wa viwanja vya michezo ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa viwanja hivyo.
Akifunga rasmi mashindano ya Imran cup yaliyomalizika jana na kushirikisha timu 7 za Manispaa ya Lindi,Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila alizitaka Halmashauri hizo kuthamini Michezo ikiwa pamoja na utengaji na Ujenzi wa Viwanja vya Michezo ili kuibua vipaji vya Wanamichezo Ili kuinua sekta ya michezo katika ngazi yoyote kama hutakuwa na
viwanja vya kutosha na vilivyo katika ubora unaostahili kwa michezo husika. Ikiwa pamoja na uwepo wa ufinyu wa bajeti ya michezo
‘’Wakurugenzi kupitia maafisa michezo nawaomba kupanga bajeti za michezo na pia lazima mtenge maeneo ya viwanja na huu wa Ilulu uboreshwe kwa kuwa ndio kioo cha Mkoa katika viwanja;;;Alisisitiza Mwananzila
image Awali akitoa taarifa ya Mashindano hayo kwa Mgeni rasmi,Mratibu wa Mashindano hayo ambae pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi,Abdulaziz Ahmeid alimuomba mkuu wa Mkoa wa Lindi kuangalia Uwezekano wa kuunda Mfuko wa kusaidia Michezo Lindi kwa kuchangisha kupitia Mazao,Mafuta na Vinywaji ikiwa Pamoja na Kuona
umuhimu wa kutenga maeneo ya Ujenzi wa Viwanja Katika Fainali hiyo Timu ya Lunduno Fc Ya Kata ya Mikumbi iliibuka kidedea na kutwaa kikombe cha Ligi hiyo pamoja na seti ya jezi baada ya Kuifunga Timu ya Kata ya Nachingwea .Manispaa ya Lindi kwa  mabao 6 kwa 5 baada ya kupigiana Mikwaju ya penalty baada ya Kumalizika kwa dakika 90 mabao yakiwa bila kwa bila
image Timu zilizoshiriki ligi hiyo ni Nachingwea fc,Brazil Fc,Makavu Fc,Kusini Soccer,Lunduno sc,Mtanda Fc na Lindi Sports zote toka Manispaa ya Lindi Fainali za ligi iliyokuwa katika sikukuu za Idd el fitr ziliendana na michezo ya kukimbia,kufukuza kuku,kukimbia na magunia pamoja na mbio za baiskeli kuzunguka uwanja wa Ilulu

About Author

Advertisement

 
Top