NIJUZE NIJUZE Author
Title: JUMUIA YA WAFANYABIASHARA YAPINGA MAANDAMANO YA CHADEMA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Hamisi Livembe akizungumza na wanahabari wa mkoa wa Lindi Januari 19, 2024 Na Ahmad Mmow, ...
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Hamisi Livembe akizungumza na wanahabari wa mkoa wa Lindi Januari 19, 2024

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Jumuia ya wafanyabiashara nchini haikubaliani na haiungi mkono  maandano yanayopangwa na kuratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) ambacho kimepanga yafanyike tarehe 24.01.2024.

Leo akizungumza  na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mjini Lindi, mwenyekiti wa taifa wa jumuia hiyo, Hamisi Livembe amesema jumuia hiyo haiungi mkono mpango huo wa CHADEMA. Kwani utakuwa na madhara kwa wafanyabiashara iwapo yatafanyika maandamano hayo.

Livembe amesema jumuia ya wafanyabiashara inatambua kwamba maandamano yanatambulika kisheria. Hata hivyo kwa upande wao wanaona yanamadhara licha ya sheria kutamka kama ni haki kuandamana.

Amebainisha kwamba uzoefu unaonesha maandamano yanatumiwa vibaya na watu waovu ambao wanatumia kutekeleza vitendo vya kihalifu. Ikiwamo kuvunja na kupora mali.

Amesema maandamano yatasababisha wafanyabiashara kufunga biashara ili kuepuka kuporwa na watu wabaya ambao watajiingiza kwenye maandamano. Hasa kwenye mitaa na barabara ambazo waandamanaji watapitia.

"Hatusemi maandamano sio haki ni kosa kwa mujibu wa sheria. Bali sisi kwa upande wetu yanamadhara bila kujali kama ni maandano halali au haramu. Mtu akifa kutokana na vurugu zilizosababishwa na maandamano itakuwa ni halali kwasababu sheria inatambua maandamano? Sisi wafanyabiasha tunaona tutapata hasara," Livembe alifafanua, kusisitiza na kuonya.

Mwenyekiti huyo wa jumuia ya wafanyabiashara abainisha na kushauri kwamba madai ya CHADEMA  hatakama yatakuwa na mashiko lakini njia ya kufikisha na kushinikiza madai hayo yafanyiwe kazi yasiwe maandamano. Bali viongozi wa chama hicho wakutane na viongozi wa serikali ili kujadili na kupata ufumbuzi wa madai hayo iwapo yana umuhimu na masilahi mapana kwa nchi.

Nae mwenyekiti wa Jumuia ya wafanyabiashara wa mkoa wa Lindi, Ahmad Mikapa aliunga mkono maelezo ya Livembe. Huku akitoa rai kwa wafanyabiashara waliopo katika mkoa wa Lindi wasishiriki wala kuunga mkono maandamano hayo.

Mikapa aliweka wazi kwamba wafanyabiashara katika mkoa wa Lindi hadi sasa hawajaonesha kuunga mkono maandamano hayo kwa njia yoyote.  Bali wanaendelea na shughuli zao huku hali ikiwa shwari  na tulivu.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimepanga kufanya maandamano ya amani ambayo lengo lake nikupinga wasilisho la serikali kuhusu muundo wa tume ya uchaguzi na mambo mengine ambayo chenyewe kinaona yanatakiwa kufanyiwa marekebisho.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top