SIMULIZI:: SITALIA TENA
SEHEMU YA 01
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
SEHEMU YA 01
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
Where do you live?” (unaishi wapi?)“Tanzania! You?” (Tanzania! Wewe?) “Oman.” “This is my first time to chart with an African girl, you look stunning...” (hii ni mara yangu ya kwanza kuwasiliana na mwanamke wa Kiafrika, umependeza) “Thank you Kaseem.” (Nashukuru Kaseem).
Msichana Saida alikuwa kwenye kompyuta yake ya mapajani akiwasiliana na mwanaume aliyekutana naye katika Mtandao wa Kijamii wa Facebook, Mwarabu aliyekuwa akiishi nchini Oman.
Muda wote uso wa Saida ulikuwa kwenye tabasamu pana. Kitendo cha kuwasiliana na mwanaume huyo kilimfanya kujawa na furaha tele huku muda wote uso wake ulitawaliwa na tabasamu pana. Kijana aliyekuwa akiwasiliana naye kipindi hicho aliitwa kwa jina la Kassem Abdulaziz. Alikuwa mwanaume wa Kiarabu aliyekuwa akiishi nchini Oman. Mara ya kwanza walikutana ndani ya Mtandao wa Facebook, japokuwa Saida alikuwa msichana mrembo aliyewaletea mapozi wanaume wengi katika mtandao huo lakini kwa Kaseem akashindwa kukataa, alipotumiwa meseji ya kwanza tu, akamjibu na kujikuta wakiwasiliana kila siku.
Moyo wake ukatokea kuvutiwa na mwanaume huyo wa Kiarabu. Alikuwa na sura nzuri, ndevu alizozinyoa kwa staili ya O huku nywele zake akiwa amezipendezesha kwa dawa za nywele zilizomfanya kuvutia na kupendeza machoni mwa msichana yeyote yule. Saida hakutaka kuishia kuangalia picha moja tu, alichokifanya ni kufungua katika sehemu ya picha za mwanaume huyo na kuanza kuangalia picha nyingine. Akatokea kumpenda lakini hakutaka kuweka wazi, waliendelea kuchati siku hadi siku, wiki hadi wiki pasipo kuonana.
Saida hakutaka kuficha, alichokifanya ni kuwaambia marafiki zake kuhusu Kaseem. Kila mmoja alimshangaa. Hawakumshangaa kwamba kwa nini alikuwa na mwanaume huyo, walichoshangaa ni kwa nini alimwamini mwanaume wa mtandaoni. Marafiki zake wakamwambia kwamba lingekuwa jambo jema kama angeachana naye lakini Saida hakutaka kusikia kwani moyo wake ulitekwa, hakuona kama angeweza kuachana na mwanaume huyo ambaye kwake, tayari alimuona kuwa mwanaume wake wa ndoto.
Alichokifanya ni kuwaonyeshea picha za Kaseem, marafiki zake hawakuamini kama kweli duniani kulikuwa na mwanaume aliyekuwa na sura nzuri kama alivyokuwa Kaseem. Nao wakajikuta wakianza kumtamani. “Ni mwanaume mzuri sana, mpaka nakuonea wivu,” alisema rafiki yake aliyeitwa Grace. Aliishikilia simu ya Saida na kuanza kuangalia picha za mwanaume huyo. “Ninampenda sana...” alisema Saida. “Umemwambia?” “Anajua hilo nadhani, ila sijamtamkia kwa maneno, naogopa,” alisema Saida na kisha kutoa kicheko kidogo.
Mawasiliano yakapamba zaidi. Kila siku ilikuwa ni lazima kuwasiliana na mwanaume huyo. Mawasiliano hayakuishia kwenye Facebook tu, wakahamia kwenye WhatsApp na kuanza kuwasiliana huko. Wakawa huru, wakatumiana sana picha mbalimbali. Kwa jinsi alivyoonekana, Kaseem hakuwa mwanaume masikini. Alikuwa akipiga picha kwenye magari mazuri, ya gharama ambayo yalimtoa udenda Saida.
Alitamani kumuuliza kuhusu familia yao lakini akaamua kunyamaza, hakutaka kuonekana kama alizipenda fedha zake, alichotaka kumuonyeshea ni mapenzi mazito, hata kama mwanaume huyo angekuwa masikini, basi angempenda hivyohivyo. “Wewe unaishi Tanzania sehemu gani?” aliuliza Kassem. “Dar es Salaam.” “Ooh! Ningependa siku nije huko nikuone. Nitaruhusiwa?” aliuliza Kaseem. “Hakuna tatizo. Karibu!”
Baada ya kuwasiliana kwa miezi mitatu ndipo Kaseem alipoamua kutupa karata yake, akaamua kumwambia Saida kile kilichoendelea ndani ya moyo wake, jinsi alivyokuwa akimpenda na kuhisi mapenzi mazito ndani ya moyo wake. Kwa Saida, hakutaka kuwa na pingamizi, alimpenda mwanaume huyo na hatimaye wakajikuta wakiingia katika dimbwi la mahaba mazito. Wakapendana sana, kwa Saida, hakutaka kuwa na mwanaume yeyote yule zaidi ya mwanaume huyo ambaye hakuwahi kuonana naye katika maisha yake zaidi ya kuona picha zake tu na video walizokuwa wakitumiana katika Mtandao wa WhatsApp. “Naomba nikwambie kitu,” alisema mwanaume huyo. “Niambie!” “Lakini naomba iwe siri! Usimwambie mtu, hasa ndugu na marafiki zako!” alisema Kaseem, kidogo Saida akashtuka.
“Hakuna tatizo!” “Umekwishawahi kumsikia mtu anayeitwa Fabrouz Abdulaziz?” “Hapana! Ndiye nani?” “Mtafute Google.” “Sawa.” Alichokifanya Saida ni kumtafuta mwanaume huyo aliyeambiwa. Kutokana na jina la mwanaume huyo kuwa kubwa, wala Saida hakupata wakati mgumu, akamuona mtu huyo na kuanza kumwangalia.
Akashtuka. Mwanaume huyo alikuwa mmoja wa mabilionea wakubwa katika nchi za Uarabuni. Alikuwa akimiliki kiasi kikubwa cha fedha, visima vya mafuta, migodi na hoteli kubwa nchini Oman. Saida hakuishia hapo, alichokifanya ni kuangalia familia ya mzee huyo. Hakuamini baada ya kuona kuwa mzee huyo bilionea alikuwa na watoto wawili tu, msichana aliyeitwa Faudhia na mwanaume aliyeitwa Kaseem, na alipofungua picha kumuona huyo Kaseem, macho yake yakatua kwa mwanaume huyohuyo aliyekuwa akiwasiliana naye.
“Kaseem...is it true?” (Kaseem...ni kweli?) “About what?” (kuhusu nini?) “What I’ve seen,” (kile nilichokiona) “Please...don’t tell anyone!” (naomba usimwambie yeyote...tafadhali)
Saida akatulia, hakuamini kama kweli alikuwa mpenzi wa mtoto wa bilionea kutoka nchini Oman. Akashusha pumzi ndefu kisha kuanza kuziangalia tena picha za Kaseem, akaangalia magari aliyokuwa akipiga picha Kaseem na nyumba aliyokuwa amesimama mbele yake, akajikuta akichanganyikiwa akili yake. “I want you to marry me,” (nataka nikuoe) alisema Kaseem. “Kaseem...” “Please...be my wife..” (naomba uwe mke wangu, tafadhali) alisema Kaseem kupitia video fupi katika WhatsApp.
************************************************ Alitoka katika familia ya kawaida, haikuwa kwenye utajiri wa umasikini. Kipindi hicho ndiyo kwanza alikuwa ameanza chuo, kitendo cha kuambiwa na Kaseem kwamba alitamani sana awe mke wake kikamchanganya.
Saida hakutaka kujibu harakaharaka, akatulia na kumwambia Kaseem kwamba alihitaji muda na angemjibu kuhusu hilo alilomwambia. Hakutaka kuwashirikisha marafiki zake, alichokifanya ni kutumia muda wake na kuanza kujiuliza kama alikuwa sahihi kumkubalia Kaseem au la.
Wakati mwingine akawa anajiuliza kama kweli Kaseem yule mtoto wa bilionea Abdulaziz alikuwa huyo aliyekuwa akiwasiliana naye au mwingine. Baada ya kujifikiria sana kuhusu hilo, baadaye akajipa jibu kwamba huyo alikuwa ndiye yeye kwani hata alipomwangalia kwenye Wikipedia, alikuwa yeye.
“Nimkubalie au? Mungu wangu! Naomba jibu lako,” alisema Saida. Ilikuwa rahisi sana kwa msichana kukubali kuwa na mtu kama Kaseem, ila kwake, kidogo moyo wake ulikuwa na hofu kubwa.
Je, nini kitaendelea?, Tukutane Leo Saa Moja Usiku Kutokana na maombi ya watu hadithi hii itawajia mara mbili kwa Siku yaani Asubuhi na Jioni.
Itakuwa inaendelea hapa na katika website hii bonyeza link=> HADITHI

Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.