WAZIRI wa Sheria na Katiba Profesa Kabudi Palamagamba amezindua rasmi siku 16 za uanaharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia wenye kauli mbiu ya kuelekea miaka 30 ya Beijing CHAGUA kutokomeza Ukatili wa kijinsia.
Akizindua uzinduzi huo jijini Dar es Salaam ambapo wadau na wanaharakati mbalimbali wameweza kushiriki uzinduzi huo,Prof. Palamagamba alisema ukatili wakijinsia unapaswa kupingwa kwa nguvu zote.
Amesema suala la ukatili wa kijinsia ni suala la aibu linalobeza kundi kubwa katika jamii na si la kifahari kulitetea.
''Suala hilo la ukatili wa kijinsia ni suala baya na linalohitaji kutokomezwa na hali budi kuchukuliwa hatua stahiki.
''Katika
sheria zetu mbalimbali tunasheria nyingi zinazopinga ukatili wa
kijinsia na zinaelezea masuala hayo na kutoa adhabu kali ikiwemo sheria
ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mkiisoma sheria hiyo imeelezea ukatili
katika maeneo mengi,'' amesema na kuongeza
''Miongoni mwa sheria
hiyo imeeleza ukatili wa kutowanunulia nguo watoto wao,kutonunua Chakula
kwa watoto ni kosa la jinai na lipo ndani ya adhabu,usipowatunza
watoto lakini pia sheria ya huduma ya msaada wa sheria sura ya 21 nayo
inazungumza utoaji wa msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto".
Amesema
licha ya Tanzania kupiga hatua katika mapambano hayo bado inahitaji
kupiga hatua zaidi na kutaka kila mmoja awe balozi wa kupinga ukatili wa
kijinsia.
''Sasa ni wakati wa kila mmoja wetu kuwa balozi wa kuhakikisha anapinga ukatili wa kijinsia kwani kunasheria mbalimbali zinatambua masuala hayo ya ukatili wa kijinsia..
Aidha alisema moja ya mambo ambayo hayapaswi kuyaacha ni kuendeleza mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia ''Niwaombe kampeni hii iwe endelevu isiishie kwenye hizi iku 16 ,Serikali itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia na utu wa wanawake,''alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi Shirika
la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF), Dk.
Monica Muhoja amesema kuna haja ya kuongeza kasi zaidi katika kumuinua
mwanamke sambamba na kutungwa kwa sheria maalum za kupinga ukatili wa
kijinsia.
Amesema wanawake na watoto wameendelea kuwa waathirika
wa vitendo hivyo na kwamba wako tayari kubainisha mapungufu yaliyopo
kwenye Sheria ya Kanuni ya Adhabu kwa kuwa walifanya utafiti.
Amesema
serikali imekuwa ikishughuļikia maombi mbalimbali wanayowasilisha hivyo
kwa mwaka huu wameomba serikali kuendelea kuyachukulia hatua maombi
wanayoyaomba kushughulikiwa .
"Mwaka huu tumekuja na maombi mengine ambapo tunaomba Serikali kuweza kuyashughulia ikiwemo ombi la kutumia
juhudi za kuwafikishia kwenye agenda za kiusalama kwa kuhakikisha kuwa
masuala ya ukatili wa kijinsia yanaingizwa rasmi katika mipango na
mikakati ya kiusalama ya kitaifa .
"Maombi mengine ni pamoja na
serikali ni kuomba kutungwa kwa sheria mahsusi ambayo italinda jamii
hasa wanawake na watoto dhidi ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.
Naye
Mkurugenzi wa WiLDAF (Women in Law and Development in Africa),Anna
Kulaya alisema dhamira ya Kampeni hiyo ni kushawishi na kuhamasisha
jamii kuondoa mitazamo inayochochea unyanyasaji na ukandamizaji wa
kijinsia huku ikikuza usawa,heshima na haki kwa wote.
“Leo ni
siku muhimu sana kwetu sote tunapoanza safari ya kuelekea Siku 16 za
Uanaharakati wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia, Hii ni fursa ya kipekee ya
kushirikiana, kuhamasisha, na kuchukua hatua za pamoja dhidi ya aina
zote za ukatili wa kijinsia kwa ajili ya jamii yenye usawa, heshima, na
haki kwa wote.
“Muungano huu ulipoanzishwa ulikuwa na mashirika
tisa tu, lakini kwa miaka kadhaa umeendelea kukua na kuvutia wanachama
wengi, kutokana na juhudi zake za pamoja za kupinga ukatili wa kijinsia
na kukuza usawa wa kijinsia katika jamii.," alisema.
Alisema
Mkuki ni harakati inayolenga kuleta mabadiliko chanya katika jamii kwa
kukuza uelewa na kubadili fikra potofu zinazoendeleza ukatili wa
kijinsia.
“Mkuki ni muungano mkubwa wa mashirika zaidi ya 200,
unaofanya kazi chini ya uratibu wa WiLDAF (Women in Law and Development
in Africa),dhamira yake kuu ni kushawishi na kuhamasisha jamii kuondoa
mitazamo inayochochea unyanyasaji na ukandamizaji wa kijinsia, huku
ikikuza usawa, heshima, na haki kwa wote.” alisema na kuongeza
"Kupitia elimu, kampeni za kijamii, na ushirikiano na wadau mbalimbali, Mkuki inalenga kuwa sauti ya mabadiliko na chachu ya jamii yenye amani, heshima, na utu kwa kila mtu bila kujali jinsia," alisema.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.