Unknown Unknown Author
Title: Vodacom yazindua Router E 5331
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imezindua kifaa kipya aina ya Router E 5331 ambacho kitauzwa kwa sh 145,999 cha kumwezesha mteja kuperuzi intan...
vodacom-red-logo-vodafone1 KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imezindua kifaa kipya aina ya Router E 5331 ambacho kitauzwa kwa sh 145,999 cha kumwezesha mteja kuperuzi intaneti bure kwa miezi mitatu na kuangalia salio kwa kupiga *149*30#.
Kifaa hicho kinatarajiwa kukidhi mahitaji ya Watanzania katika soko na kuongeza urahisi wa matumizi ya intaneti kwa gharama nafuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, alisema kuwa kifaa hicho ni mwafaka kwa watumiaji wa intaneti za masafa na kuunganisha vifaa na watumiajii mbalimbali kwa wakati mmoja.
Aliongeza kuwa kifaa hicho ni muafaka kwa matumizi ya nyumbani na  kwa wafanyabiashara wadogo ambao wanatumia kompyuta zaidi ya moja na vifaa vingine vinavyounganishwa na intaneti kwa masafa.
“Kupitia kifaa hichi cha Router E5331, watumiaji wetu wa intaneti wataweza kutumia “Vodacom Multi-Connect,”

Alisema kifaa hicho kitaunganisha watumiaji wengi na kupata intaneti yenye kasi zaidi kwa masafa popote watakapokuwa iwe ofisini au nyumbani.
Kwamba kwa kutumia Router E5331 mteja anaweza kuunganisha vifaa zaidi ya vitano kama kompyuta, mashine za photocopy, vifaa vya michezo, komputa za mapajani (Laptop) na simu zenye uwezo wa Wi-Fi.

Mteja pia anaweza kufurahia huduma ya intaneti yenye kasi ya 3G. Hii itamuwezesha kupata huduma popote atakapokuwa.
Wakati huo huo, kampuni hiyo, imeahidi kuendelea kutoa mchango wake katika sekta ya habari ili kuleta maendeleo zaidi katika sekta hiyo nchini.
Akizungumza na waandishi na wahariri wa habari wakati wa warsha kwa wamiliki Kampuni ya Capital Plus International (CPI) ya jijini Dar es Salam mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twisa alisema kuwa kampuni yake inatambua umuhimu wa vyombo vya habari katika maendeleo ya nchi.
Pamoja na mambo mengine, Twisa aliviasa vyombo vya habari kuboresha taarifa watoazo kwani pamoja na kukuza mauzo yao suala hilo litasaidia kurejesha imani kwa wasomaji na watazamaji wao.
Warsha hiyo ya siku mbili ilikutanisha wamiliki wa vyombo vya habari zaidi ya 50 na waandishi wa habari na wahariri pamoja na mameneja zaidi ya 100 ikiwa imedhaminiwa na Vodacom, Benki ya Standard Chartered, Benki ya National Microfinace (NMB), Precision Air na Hoteli ya Serena.










About Author

Advertisement

 
Top