KAGAME CUP - YANGA Vs ATLETICO

Mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) Young Africans Sports Club leo inaanza kutetea taji lake la Ubingwa huo kwa kucheza mchzeo wa ufunguzi dhidi ya timu  ya Atletico ya Burundi katika uwnaja wa Taifa jijini Dar es salaam

Young Africans ambayo kwa sasa inanyolewa na kocha mbeligiji Tom Saintfiet, itacheza na mabingwa hao wa Burundi majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Akiongea na tovuti ya klabu www.youngafricans.co.tz Kocha Mkuu Tom Saintfiet amesema vijana wake wameiva, na wanaonekana kushika mafunzo yake vizuri, hivyo wapenzi wa Yanga wanaombwa kujitokeza kwa wingi kuja kuishangilia timuyao.

Yanga ambayo ipo katika kundi C pamoja na timu za APR (Rwanda), Waal (Sudan Kusini) itakua na kikosi cha wachezaji wa 20 ambao kocha mkuu aliwatangaza kuwatumia katika mashindano hayo.

viingilio vya mchezo wa leo ni:

VIP A, 30,000/=

VIP B, 15,000/=

VIP  , 10,000/=

Rangi ya Machungwa, 7,000/=

Bluu & Kijani , 5,000/=

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post