MFUKO WA BIMA YA AFYA YATAKIWA KUJENGA HOSPITAL ZAKE KUHUDUMIA WATEJA WAKE NA WANANCHI KIUJUMLA

DSC00426
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini inabidi ujenge hospitali zake wenyewe ili kutoa huduma bora zaidi kwa wanachama waliopo na wananchi wote kwa jumla badala ya kujiegemeza tu kwenye hospitali nyingine na vituo vya afya.
 Alikuwa akizungumza katika maadhimisho ya miaka 10 ya Mfuko huo kwenye viwanja vya Ofisi Kuu ya Mfuko Kurasini jijini Dar es Salaam ambapo pia Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa alitunukiwa tuzo ya "shujaa" kwa uanzilishi wa mfuko huo. "Wakati umefika sasa kwa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya kuangalia uwezekano wa kuwekeza kwa kujenga hospitali zake yenyewe ili kuweza kutoa huduma bora zaidi kwa wanachama waliopo na wananchi wote kwa jumla," alisema.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na: 8 ya mwaka 1999 na Mfuko huo ulianza kazi mwaka 2001, ukiwa na wanchama wachangiaji wapatao 160,000  na hivi sasa una wanachama wapatao 470,000 na unawahudumia wananchi zaidi ya milioni 2.5.
Mpaka sasa mfuko huo umelipa Sh. Bilioni 140 kwa vituo vya matibabu nchini, vinavyowahudumia wanachama wa bima ya afya na wategemezi wao.
Baadhi ya wengine waliopewa tuzo ni pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Mawaziri  na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Afya waliokuwepo wakati Mfuko huo unaanzishwa.
Waziri Mkuu Pinda pia alikagua jengo la kuhifadhi majalada ya wanachama wa bima ya afya na wategemezi wao hapo hapo makao makuu ya Mfuko wa Bima ya Afya.


Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021,
DAR ES SALAAM
Jumatatu Machi 19, 2012

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post