JK AMTEUA NDOMBA KUWA MKUU WA JKT

clip_image002

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali Samwel Albert Ndomba kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia tarehe 14 March 2012.
Meja Jenerali Samwel Albert Ndomba alizaliwa tarehe 22 Apr 1954 wilaya ya Mbinga, mkoa wa Ruvuma. Meja Jenerali Ndomba aliandikishwa Jeshi mwaka 1976 na kutunukiwa kamisheni 1977.
Katika Utumishi wake amewahi kushika madarakayafuatayo, Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Jeshi, Mkuu wa Wilaya Ngara, Mkuu wa Mkoa Arusha na Mkuu wa Utumishi wa Jeshi.
Meja Jenerali Ndomba anashika nafasi iliyoachwa wazi na Meja Jenerali Samweli Kitundu ambae amestaafu kwa mujibu wa sheria.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post