Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla rasmi iliyofanyika leo, Novemba 3, 2025, katika Uwanja wa Gwaride, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, wakiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mawaziri, viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio hilo muhimu katika historia ya Taifa.
Baada ya kula kiapo, Dkt. Nchimbi ameahidi kushirikiana kwa karibu na Rais katika kuendeleza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuwaletea Watanzania maendeleo endelevu.
Tags
HABARI ZA KITAIFA

