BAADA ya uongozi wa Yanga kuamua kupitisha panga kwa baadhi ya wafanyakazi wake, akiwemo mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha klabu hiyo, Jerry Muro, kumeibuka gumzo juu ya suala hilo.
Baadhi ya wanachama wa Yanga, wamekuja juu na kuutaka uongozi wa klabu hiyo kubatilisha maamuzi yake ya kumfungashia virago Muro kwani alikuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya klabu hiyo.
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo ile inayomilikiwa na klabu hiyo, wanachama hao wamedai kuwa kama ni uongozi huo umechukua uamuzi huo wa kumfungashia virago Muro kwa sababu ya ukata ni mara kumi akapunguzwa mtu mwingine lakini siyo Muro.
Baadhi ya baadhi wanachama jana walikusanyika makao makuu ya klabu hiyo kwa lengo la kutaka kuonana na uongozi wa klabu hiyo ili usitishe zoezi hilo la kufungashia virago Muro lakini hakufanikiwa kuonana na uongozi huo.
Hata hivyo alipoulizwa Muro kama tayari ameshakabidhiwa barua ya kufungashiwa virago na uongozi wa Yanga alisema: “Sijapata barua yoyote na wala sina taarifa hizo.”
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, amedai kusikitishwa na uamuzi huo uliofikiwa na uongozi dhidi ya Muro na amedai: “Sina mengi ya kusema ila Muro anatakiwa kujua kuwa kiongozi wetu huyo hivyo ndivyo alivyo ila mchango wake ndani ya Yanga nitaendelea kuutambua.”

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.