Na Mwandishi Wetu,Muheza
RAIS Dkt..Samia Suluhu Hassan amekutana na Oryx Gas pamoja na wadau wengine ambapo wamemuhakikishia wataendelea kuunga mkono kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kupeleka mitungi ya gesi vijijini ili kuwezesha wananchi kuipata kwa urahisi.
Ametoa kauli hiyo
alipotembelea banda la Oryx Gas wakati wa uzinduzi wa kampeni ya
matumizi nishati safi ya kupikia Kitaifa iliyozinduliwa katika viwanja
vya Jitegemee wilayani Muheza mkoani Tanga.
"Mitungi ya gesi inapoisha inabaki ndani kama feniture (Samani za ndani) ,hivyo nimeomba sekta binafsi na nimekutana na Oryx Gas na wadau wengine na wakanihakikishia wataendelea kuipeleka mitungi ili wananchi waendelee kutumia.” amesema Rais Samia huku akiipongeza Oryx Gas.
Awali
akitoa maelezo kwa Rais Samia, Meneja Miradi ya Nishati Safi ya Kupikia
kutoka Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba amesema kampuni hiyo imekuwa
ikifanya jitihada mbambali za kuunga mkono kampeni ya kuhamasisha
matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini na mkakati wao ni kuona kila
nyumba inakuwa na mtungi wa gesi ya kupikia.
“Tunamshukuru Rais
Dk.Samia Suluhu Hassan kwa ajenda yake ya kuhamasisha matumizi ya
nishati safi ya kupikia. Oryx Gas tumekuwa wadau wakubwa na tumefanya
jitihada nyingi tokeo ilipotangazwa kama ajenda rasmi ya nchi kwamba
wananchi tuanze kutumia nishati safi ya kupikia
“Tumeongeza
miundombinu ya kusambaza mitungi ya Oryx Gas hasa katika maeneo ya
vijiji ambapo kwa sasa huwezi kuikosa Oryx gas. mitungi ya Oryx
inapatikana kila miji,Wilaya na vijijini pia tupo. Pia tumekuwa
tukishiriki katika shughuli za mbalimbali za kuwezesha ukuaji wa
matumizi ya nishati safi ambapo tumeweza kuisaidia jamii mbalimbali
ikiwemo ya Wanawake kwa kuiwezesha kufikia hayo malengo.