Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameeleza kuwa Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetumia jumla ya shilingi trilioni 8.2 kugharamia masomo ya wanafunzi tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo.
Waziri Mkuu alibainisha kuwa, katika kipindi hicho, wanafunzi takribani 830,000 wamefaidika na mfumo huu wa ugharamiaji wa elimu ya juu kupitia Bodi ya Mikopo.
Majaliwa aliyasema hayo Jumatatu, Februari 17, 2025, alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu. Sherehe hizo zilifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Tags
HABARI ZA KITAIFA